RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Jaffar Mohamed Haniu kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu). Anaripoti Jemima Samwel, DMC … (endelea).
Taarifa ya uteuzi huo wa Haniu, imetolewa leo Jumatano, tarehe 9 Juni 2021 na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, anayemaliza muda wake.
Msigwa ambaye tayari ameteuliwa na Rais Samia kuwa Mkuruegnzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, amesema, uteuzi wa Haniu unaanza leo Jumatano.

Kabla ya uteuzi huo, Haniu ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari, alikuwa Mtendaji Mkuu wa vyombo vya habari vya Africa Media Group Limited vya Channel Ten na Magic FM.
Leave a comment