June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

IGP Sirro azungumzia tuhuma za Mbowe, atoa onyo

Spread the love

 

INSPEKTA Jenerali wa Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro amekitaka chama kikuu cha upinzani nchini humo, Chadema na wadau wengine, kuiachia mahakamana kesi inayomkabili mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mbowe na wenzake watatu, wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwemo la kupanga njama za ugaidi na uhujumu uchumi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Tangu kukamatwa jijini Mwanza na kusafirishwa hadi Dar es Salaam na kisha kufikishwa mahakamani, wadau mbalimbali wa kutetea haki za binadamu wa ndani na nje ya Tanzania, wamekuwa wakipinga suala hilo.

Wameitaka dola kumwachia Mbowe aliyekamatwa usiku wa manane, akiwa hotelini kabla ya kushiriki kongamano la Katiba mpya ambalo hata hivyo halikufanyika.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Leo Jumatatu, tarehe 2 Agosti 2021, IGP Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema, Mbowe na wenzake wamefikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Sirro amewaonya wale wote wanaokusudia kufanya maandamano tarehe 5 Agosti 2021, siku ambayo kesi hiyo itatajwa tena kutokufanya hivyo kwani “kuvamia mahakama ni sawa na kuvamia kambi ya jeshi, utakung’utwa tu, hivyo tuiachie mahakama ifanye kazi yake.”

“Chadema wanasema mwenyekiti wao (Mbowe) ameonewa, wanavyoona wao hawezi kufanya hivyo, sasa kama Mbowe ni mkweli na amamuamini Mungu waende wakamuulize jambo hili unasemaje.”

“Lakini kabla ya uchaguzi nilisema kuna watu wamepanga kuhakikisha uchaguzi haufanyiki, nilisema kuna watu wamepanga kulipua visima vya mafuta na nilisema wamepanga kuua viongozi na nilisema tutawakamata,” amesema Sirro

“Habari ya yeye wajue ni binadamu, anaweza kufanya makossa. Walitafuta vijana wetu tuliowafukuza jeshini, tumempeleka mahakamani tuwache mahakama itimize wajibu wake, habari za chama cha siasa, habari za viongozi wa dini, asasi za kiraia waache,” amesema Sirro

Katika kusisitiza hilo, Sirro amesema, “kama kweli ni mkweli mwenyekiti wao, na amaanimi Mungu waende wakamuulize, lakini wengine wanaosema sema ni sawa na jambo usilolijua ni kama usiku wa giza, usiingie katika mtego, tusubiri mahakama ifanye kazi yake.”

Sirro amewaonya wanaotaka kuhatarisha usalama wa nchi kwamba serikali haitawaacha salama na “tuwaache wale watu wachache wanaotaka kupambana na serikali, lakini kama wameandaa kwenda Canada, Marekani waende ila hatutaruhusu kikundi cha watu.”

“Wale ambao wameambiwa wakusanyike kuja mahakamani, waelewe mahakaman ni eneo nyeti, Mahakama ni sawa na kituo cha polisi, ukitaka kuvamia utakung’utwa, Mbowe yuko mahakamani waiache ifanye kazi zake,” amesema

error: Content is protected !!