May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yavuta mwengine

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Yanga, imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji Yusuph Athuman Akitokea klabu ya Biashara United, Mara iliyokuwa inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mshambuliaji huyo ameingia mkataba wa miaka mitatu, kukipiga ndani ya Yanga ambapo alikuwepo hapo awali kwenye timu ya vijana.

Kwenye msimu wa 2020/21. Akiwa na kikosi cha Biashara United Yusuph alicheza jumla ya dakika 216, na kufanikiwa kufunga mabao 2, na kutoa pasi za mabao (assist) mbili.

Huu utakuwa usajili wa pili wa Yanga, ndani ya siku mbili mara baada ya kumtambulisha mshambuliaji kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Fiston Kalala Mayele.

Klabu hiyo inaendelea kuimarisha kikosi chake katika kuelekea msimu ujao wa mashindano, hasa Ligi Kuu Tanzania Bara, na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

error: Content is protected !!