Thursday , 23 March 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Majaliwa atoa maagizo wanufaika mafunzo ya ufundi
Elimu

Majaliwa atoa maagizo wanufaika mafunzo ya ufundi

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka vijana waliopata ufadhili wa Serikali kupitia programu maalum ya kupata mafunzo ya ufundi stadi watumie vizuri fursa hiyo ili wanufaike. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fungu la fedha kwa ajili ya kuwasomesha vijana katika fani mbalimbali za ufundi stadi kwa muda wa miezi sita.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana Jumapili, tarehe 1 Agosti 2021, wakati wa uzinduzi wa chuo cha Ufundi Stadi kilichopo katika kijiji cha Kipapa kata ya Lufilyo wilaya ya Busokelo mkoani Mbeya.

“Kilichotuleta hapa ni kuja kushuhudia vijana wetu wa Kitanzania ambao wameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa lengo la kuwapatia ujuzi ili wakaendeleze kazi hizo.”

Alisema Tanzania nzima kuna vijana takribani 45,000 ambao wamesambazwa katika vyuo vyote vya Serikali na vya binafsi ambapo watapatiwa mafunzo ya ufundi stadi kwa miezi sita.

Majaliwa alisema, mbali na kupatiwa ujunzi katika vyuo hivyo pia vijana wengine wamepelekwa kwenye maeneo ya kutolea huduma kama za utalii, hoteli ili wapate ujuzi.

Alisema chuo hicho cha VETA Busokelo ni kimojawapo kati ya vyuo walivyovichagua ili kipokee vijana wa maeneo ya wilaya za Rungwe, Kyela, Chunya na Mbeya ili kuwapa ujuzi.

“Matarajio yangu vijana wote waliopata nafasi hii hawataipoteza, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anatamani kuona kila Mtanzania akijishughulisha na shughuli za ujasiriamali.”

Alisema mkakati wa Serikali kwa mwaka 2021 ni kusomesha vijana 80,000 ambapo asilimia 60 ya mafunzo hayo watayapata kwa vitendo na asilimia 40 watafundishwa darasani.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Pancras Bujulu alisema chuo cha Ufundi Stadi cha Busokelo kimedahili wanafunzi 127 ambao watapa mafunzo ya ufundi kupitia program hiyo.

Alisema kati ya wanafunzi hao 26 wanasomea ufundi seremala, 45 ushonaji nguo, 28 umeme wa majumbani, 18 ukarabati wa vitarakimishi na 10 utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki.

Alisema mafanikio ya programu hiyo ni pamoja na kuwawezesha wanafunzi waliopata ujuzi kuweza kujiajiri katika fani za useremala, ushonaji, udereva na matumizi ya vitarakinishi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini wamwaga mamilioni ujenzi maabara za sekondari

Spread the love  MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara,...

ElimuHabari

CBE yaanzisha Shahada 10 za Uzamili, CBE yajivunia wahitimu wanaoajirika

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimewataka wenye  kampuni na...

Elimu

Harambee ujenzi sekondari za Musoma Vijijini yashika kasi

Spread the love  HARAMBEE ya ujenzi na ukarabati wa shule za sekondari...

Elimu

Shule ya Alpha yazindua mfumo wa kugundua vipaji vya watoto

Spread the love  SHULE ya Sekondari ya Alpha ya jijini Dar es...

error: Content is protected !!