Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Huu hapa mchakato wa uteuzi wa majaji nchini
Habari Mchanganyiko

Huu hapa mchakato wa uteuzi wa majaji nchini

Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma
Spread the love

 

JAJI mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, amesema mitandao ya kijamii haitoi taarifa sahihi kuhusu namna au utaratibu ambao wanautumia kupata majaji na hivyo kulazimika kutolea ufafanuzi jambo hilo. Anaripoti Apaikunda Mosha TUDARCO … (endelea).

Ameyazungumza hayo leo Jumatatu ya tarehe 29 Agosti 2022 katika hafla iliyofanywa na Rais Samia ya kuwaapisha majaji na kamishna jenerali wa magereza iliyofanyika Ikulu Dodoma.

Amesema kuwa Ibara ya 109(1) ya Katiba imetoa idadi ya chini kabisa ya majaji ambao wanatakiwa kuwa mahakama kuu ambao ni majaji 30 na zaidi ya hapo inatokana na mahitaji ya mahakama.

Amesema mchakato wa kuwapata Majaji hao unaanza kwa kuwaomba wadau katika sekta ya sheria ndani ya mahakama na taasisi za umma wapendekeze majina. Na majina hayo yanapelekwa katika Tume ya Utumishi wa Mahakama na kupitiwa ili kupata majina ya kupelekwa kwa Rais.

Ameeleza kuwa jumla ya majina yaliyopendekezwa wadau ni majina 232, ambayo yalipitiwa, kuangalia sifa na vigezo yakabaki majina 57, ambayo yalijumuishwa na majina ambayo yapo kwenye kanzi data ya mahakama ambao tayari wana sifa na walikuwa wanasubiri uteuzi.

Ametoa machanganuo wa majina yaliyopendekezwa na wadau kuwa 87 walitoka ndani ya mahakama, 30 walikuwa mawakili wa serikali, 22 kutoka vyuo vya juu, mawakili wa kujitegemea 53 na wizara, idara na taasisi za umma walikuwa 40 na kufanya jumla ya 232.

Amefafanua zaidi kuwa Tume ilifanya uchambuzi na kuwasilisha majina 77 kwa Rais kutokana na vigezo walivotumia kuwachagua na Rais akateuwa majina 22 ambapo 21 wameapishwa na mmoja yupo katika matibabu.

Aidha, ameainisha vigezo walivyotumia ikiwa ni pamoja na uadilifu, lugha na uwezo wa kujieleza, ujengaji wa hoja, miaka chini ya mitatu kufika umri wa kustaafu na uzoefu katika shughuli za kisiasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NBC yapata tuzo ya mwezeshaji bora wa mikopo serikali Afrika

Spread the loveBenki ya NBC imepata tuzo ya Mwezeshaji Bora wa Pamoja...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!