Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Azam FC wambadilishia majukumu kocha wao
Michezo

Azam FC wambadilishia majukumu kocha wao

Spread the love

 

MATAJIRI wa jiji la Dar es Salaam – Azam FC leo tarehe 29 Agosti, 2022 wamethibitisha kumbadilishia majukumu kocha wao mkuu, Abdihamid Maollin na Msaidizi wake, Omary Nasser kutokana na kile kilichodaiwa kuwa mwenendo usioridhisha wa timu hiyo. Anaripoti Damas Ndelema, Dar es Salaam … (endelea).

Kupitia taarifa iliyotolewa na ukurasa wa Instagram wa timu hiyo imeeleza kuwa wamefikia makubaliano baina ya pande zote mbili kati ya uongozi wa timu na makocha hao amabapo wataachia ngazi kama kocha mkuu na kocha msaidizi lakini wataendelea kubaki kuwa sehemu ya klabu hiyo.

Wawili hao wanatarajiwa kupewa majukumu mengine tofauti katika idara ya ufundi ambapo nafasi hizo zitatangazwa hapo badae

Kocha huyo alijiunga na Azam msimu uliopita wa 2021/22 akichukua mikoba ya George Lwandamina na kuisaidia Azam kufika fainali ya kombe la mapinduzi na kupoteza dhidi ya Simba.

Pia walifanikiwa kufika nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Azam na kutolewa na Coastal Union na kufanikiwa kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi kuu ya NBC.

Aidha, klabu hiyo itakuwa chini ya kocha wa makipa Daniel Cadena ambae ni kocha wa makipa mwenye leseni ya juu kabisa ya ukocha UEFA Pro Licesence hivyo ataiongoza timu hiyo mpaka pale uongozi utakapomtangaza kocha mpya.

Mpaka sasa msimu huu kwenye Ligi kuu ya NBC, Azam wamecheza mechi mbili na kushinda mechi moja dhidi ya Kagera Sugar na kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Geita Gold.

Wenyeji hao wa Chamanzi wanatarajiwa kurejea tena uwanjani tarehe 6 Septemba mwaka huu dhidi ya Yanga katika uwanja wa Benjamini Mkapa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!