September 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Hukumu kesi ya Yanga vs Morrison CAS, kutolewa ndani ya siku 26

Bernard Morrison

Spread the love

 

MAHAKAMA ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kimichezo (CAS), itatoa hukumu ya kesi ya rufaa kati ya klabu ya Yanga na mchezaji, Bernard Morrison baada ya kumaliza kusikilizwa kwa shauli hilo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea). 

Kesi hiyo ambayo ilisikilizwa siku leo, kwa njia ya mtandao kwa pande zote mbili, kati ya mdai ambao ni klabu ya Yanga na mdaiwa ambaye ni Bernad Morrison.

Taarifa juu ya mwenendo wa kesi hiyo ilitolewa na klabu ya Yanga, kupitia taarifa yao waliotoa hii leo ambayo ilikuwa inaeleza kuwa kesi hiyo imeshamaliza kusikilizwa na mahakama hiyo na CAS itatoa hukumu kwa mujibu wqa taratibu zake kuanzia siku ya jana mpaka Agosti 24 mwaka huu.

Shauri hilo liliendelea baada ya CAS kuondoka pingamizi la awali (Preliminary Objection) lililowekwa na Bernard Morrison kwa kutaka kesi hiyo kusikilizwa nchini.

Kufuatia kuondolewa kwa pingamizi hilo Juni 2 mwaka huu, Mahakama hiyo ilitaka pande zote mbili kutuma mapendekezo ya namna gani kesi itasikilizwa, kwa kutumia njia ya nyaraka au maneno (mtandao).

Morrison aliingia kwenye mgogoro na klabu hiyo mara baada ya kujiunga na klabu ya Simba Agosti, 2020 huku klabu ya Yanga ikidai kuwa bado ilikuwa na mkataba na mchezaji huyo.

Kesi hiyo ilifika kwenye kamati ya Sheria na hadhi kwa wachezaji iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake Elias Mwanjala ambao walitoa maamuzi ya kuwa mchezaji huyo yupo huru na halali kuichezea klabu ya Simba.

Mara baada ya hapo klabu ya Yanga haikulizika na hukumu hiyo na kuamua kukimbilia kwenye mahakama hiyo ya kimataifa ya michezo.

Morrison alifika nchini kwa mara ya kwanza tarehe 15 Januari, 2020 na kujiunga na Yanga kwa mkataba wa miezi sita licha ya baadae klabu hiyo kudai kuwa mchezaji huyo aliongeza tena mkataba kwa miaka miwili.

error: Content is protected !!