Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Haya hapa majina wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2024
ElimuTangulizi

Haya hapa majina wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2024

Mohamed Mchengerwa
Spread the love

Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa ametangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2024 katika shule mbalimbali za serikali nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akitangaza majina hayo leo jijini Mwanza, Mchengerwa amesema uchaguzi wa majina hayo ulihusisha wanafunzi 1,092,984 wakiwemo wasichana 507,933 na wavulana 585, 051 ambao walifaulu mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka 2023.

Katika taarifa yake kwa umma aliyoitoa kwenye mkutano wake na viongozi wa ngazi za Mikoa na Wilaya, uliofanyika ndani ya ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mchengerwa amesema vigezo vilivyotumika kuchagua wanafunzi hao ni kwa kuangalia waliopata alama za ufaulu kati ya 121 hadi 300, miongoni mwao hakuna asiyepangiwa shule.

“Idadi ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2024 imeongezeka kwa wanafunzi 16,947 sawa na ongezeko la asilimia 1.57 ikilinganishwa na wanafunzi 1,076,037 waliopata alama za kuwawezesha kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023.” Amesema Mchengerwa.

Amesema miongoni mwa waliofaulu na kupangiwa kujiunga na Kidato cha Kwanza Januari, 2024 wamo wanafunzi wenye mahitaji maalum 3,587 ambapo wasichana 1,590 na wavuala 1,997.

Aidha amesema wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika Shule za Serikali kutwa na bweni hakuna atakayekosa nafasi kwani imetenga Sh 140.5 bilioni kwaajili ya ujenzi wa madarasa mapya sambamba na ukarabati wa madarasa yaliyopo kuelekea muhula mpya wa masomo utakaoanza Januari 08, 2024.

Angalia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2024 hapa

https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/selection/psle_selection.htm

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!