Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga
Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love

 

MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia leo, Jumamosi tarehe 4 Februari, mkoani Tanga, yametajwa.

Majina hayo ni ya ndugu, familia na ukoo wa Athanas Cosmass Mrema, aliyefariki dunia jijini Dar es Salaam na basi lililobeba mwili wake kuelekea Rombo mkoani Kilimanjaro, kupata ajali jiji Tanga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga … (endelea).

Akizungumza na MwanaHalisi Online, ndugu wa marehemu Athanas Mrema, Novatus Tarimo amewataja watoto wa marehemu ambao wamefariki kwenye ajali hiyo kuwa ni Augustina Athanas Mrema na Nestory Athanas Mrema.

Amewataja ndugu wengine kuwa ni Lizybetha Linus Lamasey, Elizabeth Edward Mrema, Godwin Henry Mrema, Kenedy Joseph Mrema, Avelina Cosmas Mrema, Emiliana Colman Mrema, Rozina Andrea Lamosai, Suzana Matei Mrema, Julietha Edward Mrema na Ethan Peter.

Katika ajali hiyo miongoni mwa waliofariki, ni wanaume tisa na wanawake sita, wakiwamo watoto wawili mmoja wa kike na mmoja wa kiume.

Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 4:30 usiku, eneo la Magila Gereza, katika barabara ya Segera – Buiko, lilihusisha gari aina ya Fuso na basi dogo aina ya Toyota Coaster, iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Rombo, mkoani Kilimanjaro.

 

Basi hilo, lililokuwa na abiria 26, lilikuwa limebeba mwili wa Athanas Cosmass Mrema, aliyefariki dunia, katika Hospitali ya Bochi, iliyopo eneo la Kwa Msuguri Kata ya Saranga wilayani Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Omary Mgumba, alidai kuwa chanzo cha ajali hiyo, ni uzembe wa dereva wa lori wa kuendesha gari lake kasi kwa kutaka kulipita gari la mbele bila ya kuchukua tahadhari, hivyo kugongana uso kwa uso na basi hilo.

Kwa mujibu wa Mgumba, miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Korogwe; majeruhi 10 kati ya 12 wamehamishiwa hospitali kuu ya mkoa wa Tanga (Bombo) na wawili wamebakishwa hospitali ya Korogwe kuendelea na matibabu.
Alisema, bado kuna miili ambayo haijatambulika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania yakabidhi rasmi msaada nchini Malawi

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Bashe: Tumeshagawa pikipiki 5,500 kati ya 7,000 kwa maafisa ugani

Spread the love  WAZIRI wa Kilimo, Hussen Bashe, amesema wizara hiyo tayari...

Habari Mchanganyiko

Spika Tulia awapa neno mawaziri utekelezaji mashamba ya pamoja

Spread the love  SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amewataka mawaziri kushirikiana...

Habari Mchanganyiko

Ukosefu wa maadili kwa wakunga, wauguzi bado changamoto

Spread the loveIMEELEZWA kuwa vitendo vya uvunjifu wa maadili kwa  wauguzi na...

error: Content is protected !!