Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Papa Francis kukutana na wahanga wa vita Sudan Kusini
Kimataifa

Papa Francis kukutana na wahanga wa vita Sudan Kusini

Spread the love

 

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo Jumamosi atakutana na wahanga wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini katika siku ya pili ya ziara yake kwenye taifa hilo linalokabiliwa na machafuko. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Mkutano huo unafuatia wito alioutoa Papa Francis jana Ijumaa kwa viongozi wa Sudan Kusini akiwataka kutafuta amani ya kudumu na kukomesha mateso yanayowakumba raia.

Papa Francis aliyewasili nchini Sudan Kusini jana tarehe 3 Februari 2023 akitokea Kongo DR, amefanya mazungumzo na Rais Salva Kiir wa nchi hiyo hapo na kutoa wito wa amani.

Papa Francis amewataka viongozi wa taifa hilo changa kupambana bila kuchoka kusaka amani na kumaliza machafuko nchini humo yanayosababisha madhila ya kila siku kwa raia.

Baba Mtakatifu amekaririwa akimweleza Rais Kiir “Hakuna tena nafasi ya kufanya uharibifu na badala yake taifa hilo lianze kazi ya kujijenga.”

Rais Kiir alikuwa pamoja na hasimu wake wa muda mrefu ambaye ni Makamu wa rais wa nchi hiyo, Riek Machar wakati alipomkaribisha Papa Francis kwenye bustani ya ikulu ya rais mjini Juba.
Kiongozi huyo wa kiroho amewarai viongozi hao hadharani kukomesha umwagikaji wa damu, machafuko na uhasama.

Rais Kiir na hasimu wake Machar walikuwa wageni wa Papa Francis mjini Vatican mwaka 2019 na wakati huo Baba Mtakatifu aliwasihi kuisaka amani na alionesha kitendo cha heshima kubwa kwa kuibusu miguu ya wanasiasa hao wawili.

Kiir na Machar walifanikiwa baadaye kufikia makubaliano ya amani lakini yalisambaratika na machafuko yakazuka upya kwenye taifa hilo changa la Afrika Mashariki.

Kwenye mazungumzo na viongozi hao Papa Francis alipendekeza njia mpya ya kuharakisha mchakato wa maridhiano.
Ametoa wito wanasiasa hao kuzuia kuingizwa kwa silaha nchini Sudan Kusini akisema taifa hilo linahitaji vingi vya muhimu badala ya zana za maangamizi.

Pia alipigia upatu umuhimu wa kuimarishwa kwa sera za afya na miundombini ya Taifa hilo. Sudan Kusini mara kadhaa imeorodheshwa kuwa moja ya mataifa masikini zaidi ulimwenguni.

Miaka ya vita vya wenyewe kwa wenye imewaacha raia wake katika hali ngumu ya maisha huku wakikosa huduma za msingi za jamii.

Kwa upande wake Rais Kiir ameahidi kuanzisha tena kile kinachofahamika kuwa mazungumzo ya mjini Roma pamoja na makundi ya waasi ambao hawautambui mkataba wa amani uliotiwa saini.
Amesema anatumaini wabunge wa nchi hiyo kutoka upande wa upinzani watamuunga mkono kufanikisha upatikanaji amani.

Kuelekea ziara ya Baba Mtakatifu, raia nchini Sudan Kusini walikuwa na matumaini makubwa kuwa kiongozi huyo wa kiroho atasaidia kupunguza mivutano inayoligubika taifa hilo.

Licha ya kuwepo utulivu ndani ya serikali, bado kumekuwa na matukio ya machafuko yanayozuka mara kwa mara ndani ya nchi hiyo.

Ziara ya Papa Francis imevutia watu kutoka kila pembe ya nchi hiyo ambao wamesafiri hadi kwenye mji mkuu Juba, wengi wakiwa na matumaini ya kushuhudia kuhuishwa kwa wito wa kuwepo amani.

Kwenye ziara hiyo Papa Francis amefuatana na Askofu Mkuu wa Canterbury na mkuu wa kanisa la Anglikana Justin Welby na kiongozi wa kanisa la Scotland, Iain Greenshields.

Ziara hii inayoitwa iliyopewa jina la “Hija ya amani” ni ziara ya kwanza kabisa ya Papa Francis nchini Sudan Kusini tangu taifa hilo lenye Wakristo wengi kupata uhuru kutoka kwa Sudan yenye Waislamu wengi mwaka 2011 baada ya miongo kadhaa ya migogoro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Nyumba ya babu yake Makamu wa Rais wa Marekani yatafutwa Zambia

Spread the love  KAMALA Harris, makamu wa rais wa Marekani, amepanga kutembelea...

Kimataifa

Benki ya Uswizi mbioni kuziwekea vikwazo akaunti za siri za Wachina

Spread the love  WAKATI Serikali na Benki ya Uswizi ikichukua hatua kali...

Kimataifa

Netanyau asitisha mipango yenye utata marekebisho mfumo wa sheria

Spread the love  WAZIRI Mkuu wa nchini Israel, Benjamin Netanyahu amesema atachelewesha...

Kimataifa

Raila ahutubia waandamanaji, mabomu yarindima

Spread the loveMSAFARA wa kiongozi wa Azimio la Umoja-One Kenya, Raila Odinga...

error: Content is protected !!