Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha
Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the love

MAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wanatarajia kushiriki maandamano ya amani yaliyoandaliwa na chama hicho, kudai katiba mpya na kupinga ugumu wa maisha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 26 Februari 2024 na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalim, akielezea maandalizi ya maandamano hayo yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumanne, jijini Arusha, ambapo amesema yamefikia asilimia 97.

Mwalim amesema watu 1,000 jamii ya kimasai ni miongoni mwa washiriki wa maandamano hayo, ambao watayatumia kupaza sauti zao kupinga zoezi la Serikali kuwahamisha katika hifadhi ya Ngorongoro.

Mbali na wamasai, Mwalim amesema watu 1,800 kutoka mkoa wa Kilimanjaro na 2,300 kutoka Manyara, ni miongoni mwa waliojisairi kushiriki maandamano hayo ya hiari.

“Jamii ya wamasai zaidi ya 1,000 ambao watatoka eneo la Ngorongoro, Simanjiro na Tanga walikopelekwa ambao wamejiandikisha kushiriki maandamano hayo. Wengine ni jamii kubwa ya wafanyabiashara ndogo na wa kati Arusha,” amesema Mwalim na kuongeza:

“Mafuriko hayo yataonyesha haja na kiu ya matumaini ya watanzania wanayotaka. Yatabeba kielelezo halisi cha ugumu wa maisha, madai ya katiba mpya na miswada mitatu ambayo imepitishwa bungeni.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!