Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Hakainde Hichilem; tajiri anayetinga Ikulu Zambia, alidaiwa Freemason
KimataifaMakala & UchambuziTangulizi

Hakainde Hichilem; tajiri anayetinga Ikulu Zambia, alidaiwa Freemason

Hakainde Hichilem
Spread the love

 

ZAMBIA wameamua! Usiku wa tarehe 15 Agosti 2021. Zambia wameandika historia ya kipekeee baada ya Hakainde Hichilem, Mgombea wa chama cha upinzani cha United Party for National Development (UPND) kutangazwa mshindi wa urais na kuwa rais tajiri aliyetinga ikulu.

Hichilem amemuangusha Edger Lungu aliyekuwa akitetea nafasi hiyo baada ya kupata kura milioni 2.8 dhidi ya milioni 1.8 alizopata Lungu.

ELIMU
Hichelim alizaliwa tarehe 4 Juni 1962 huko Kusini mwa Zambia katika wilaya ya Monze. Baada ya kupata elimu ya msingi na sekondari katika eneo alikozaliwa, mwaka 1982 alijiunga na Chuo Kikuu cha Zambia kwa ufadhili wa serikali na kuhitimu mwaka 1986 ambapo alipata Shahada ya Sanaa (BA) katika Uchumi na Biashara.

Baadaye alipata shahada ya uzamili ya somo la Fedha na Biashara (MBA) kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza.

UTAJIRI

Hichilema anajulikana kwa upendo na jina lake la utani kama HH, ndiye tajiri namba moja nchini Zambia ambapo kwa mujibu wa ripoti ya jarida la Forbes iliyotolewa Juni mwaka huu, anakadiriwa kuwa na utajiri wa Dola za Marekani milioni 389 karibu Sh trilioni moja.

Utajiri wake unatokana na biashara zake ndani na nje ya Zambia. Pia ni mfugaji wa pili mkubwa nchini Zambia kwa kuwa na mifugo karibu 100,000 katika mashamba yake manne. Ni mmoja wa wauzaji wakubwa wa nyama kwa soko la ndani la Zambia, na pia mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa zaidi nchini Zambia wanaouza nje ya nchi bidhaa zitokanazo na nyama ya ng’ombe.

Pia, ana uwekezaji mkubwa katika sekta ya utalii ya Zambia.

Kutokana na elimu yake ya chuo kikuu, Hichilema alipanda katika nafasi za juu katika ajira kwenye mashirika nchini Zambia, akipata kazi za kifahari kama Mkurugenzi wa kampuni ya Coopers na Lybrand akiwa na umri wa miaka 32, kutoka 1994 hadi 1998, na baadaye kama mrithi wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Cooper, Grant Thornton, kutoka 1998 hadi 2006.

Alikuwa pia mkubwa zaidi katika kampuni mbili zinazomilikiwa na wageni ikiwa ni pamoja na Benki ya Barclays Zambia.

Aidha, Hichilema ni mtaalamu wa majadiliano ya Biashara, na ni mwanachama wa Taasisi ya Wakurugenzi ya Zambia.

FREEEMASON
Licha ya kuwa ni msabato, mwaka 2014 alituhumiwa kujihusisha na masuala ya imani Ki-Freemason.

Mmoja wa maaskofu maarufu kutoka kanisa la Orthodox nchini humo, Edward Chomba alidai kuwa ana ushahidi wa kutosha kuhusu madai yake kwamba HH amejisajili na imani hiyo isiyoamini dini yoyote.

Hata hivyo, mwaka 2017 Hichilema aliibuka na kukanusha madai hayo ambaye pia yalihusisha na baadhi ya alama zilizopo katika nembo ya chama chake.

Hichilema alidai kuwa anaheshimu imani zote hivyo yeyote atakayendelea kusambaza uzushi huo atampeleka mahakamani.

KIFUNGO GEREZANI

Katika harakati zake za kuwania kuingia Ikulu, HH alionja joto la gerezani baada kutupwa nyuma ya nondo kwa tuhuma za kuisaliti nchi yake na kutaka kumuua rais aliyekuwa madarakani wakati huo Edger Lungu.

Tarehe 11 Aprili 2017, Hichilema alitupwa korokoroni na kukaa kwa muda wa miezi minne kabla ya Ofisi ya Mwendesha mashtaka wa nchi hiyo kumwachia huru kupitia hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo yaani ‘nolle prosequi’.

Katika mahojiano aliyofanyiwa kwenye kipindi cha Hardtalk alisema, HH alisema alikaa mahabusu kwa siku nane pasina kupewa chakula, maji, kuona mwanga na isitoshe alipuliziwa maji ya pilipili kwenye sehemu zake za siri.

MGOMBEA MARA TANO

Hichilema ameibuka mshindi wa nafasi hiyo urais baada ya kujitosa kugombea mara tano mwaka 2006, 2008, 2011 na mwaka 2016 ambazo zote alishindwa.

MALENGO YAKE

Rais huyo mteule anasema ana shauku ya kuboresho mfumo wa elimu wa Zambia ili kila Mzambia mchanga apate fursa aliyopata ya kupokea msaada wa serikali ambao umewawezesha vijana kujiajiri na kukua kiuchumi.

Imeandaliwa na Gabriel Mushi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

error: Content is protected !!