May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yang’oa beki KMC

Spread the love

Klabu ya simba imekamilisha usajili wa beki wa pembeni kutoka klabu ya KMC Israel Patrick Mwenda mwenye umri wa miaka 21. Anaripoti Mintanga Hunda Tudarco…(endelea)

Mchezaji huyo ametambulishwa hii leo Agost 16, 2021 kupitia kurasa ya klabu ya simba inayopatikana kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram

Mwenda ametambulishwa huku akiwa sehemu ya kikosi cha simba kilichokua kambini Rabat, Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2021/22.

Mlinzi huyo wa kulia ambaye pia alikua nahodha wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23  amekwenda  kuchukua nafasi ya David kameta (Duchu) ambaye ametolewa kwa mkopo .

Usajili wa beki huyo unakwenda kutimiza idadi ya wachezaji 9 waliosajiliwa na simba mpaka sasa, huku baadhi yao wakiwa hawajatambulishwa.

 

 

 

 

 

error: Content is protected !!