Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko GSM atoa vielelezo umiliki eneo Makonda analodai lake
Habari Mchanganyiko

GSM atoa vielelezo umiliki eneo Makonda analodai lake

Spread the love

MFANYABISHARA Ghalib Said Mohamed maarufu GSM, ametoa vielelezo kadhaa vinavyoonesha kuhusika katika umiliki wa eneo lenye mgogoro baina yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kusambaa kwa video ambayo Makonda alionekana akidai kuwa eneo hilo ni la kwake huku akiwa amezingirwa na watu akiwemo askari aliyevalia sare za jeshi la polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi tarehe 12 Machi 2022, Mwanasheria wa GSM, Alex Mgongolwa, amesema mteja wake amempa maelekezo ya kukanusha umiliki wa Makonda na kuchukua hatua zaidi ikwemo kwenda mahakamani endapo ataendelea kudai eneo hilo ni lake.

“Leo tumewaita hapa ili kuwapa taarifa fupi ya uhalali wa umiliki wa eneo lenye Plot namba 60 lililopo Regent Estate Manispaa ya Kinondoni, Dar Es Salaam,” amesema Mgongolwa.

Mgongolwa amesema Mohammed alinunua ardhi hiyo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya makazi tarehe 21 Novemba 2006 na kuonyesha waandishi wa habari nyaraka za udhibitisho.

Amesema Tarehe 19 Septemba 2017, Mohammed aliingia Mkataba na Kampuni ya ujenzi iitwayo Group Six International wenye thamani ya Sh 640 milioni “na hii ni nakala ya Mkataba huo.”

Aidha, ameongeza kuwa mteja wake aliomba kibali cha ujenzi na Manispaa ya Kinondoni walitoa kibali cha ujenzi tarehe 16 Oktoba 2017 chenye kumbukumbu namba 00020032 kwa Ghalib Said Mohammed kwa ajili ya kuanza ujenzi wa eneo hilo.

“Baada ya kibali kutolewa, Group Six walianza ujenzi na walipeleka maombi ya malipo ya awali ya ujenzi tarehe 31 Januari 2018 na Ghalib Said Mohammed alitekeleza sehemu ya Mkataba kwa kulipa kiasi cha Sh 51.9 milioni na kuna kithibitisho cha risiti ya TRA,” amesema.

2 Comments

  • Viwanja haviuzwi. Unakodishiwa kwa mtu binafsi kwa miaka 99.
    Ningependa kampuni zipewe miaka 20 tu, na kurenew baada ya ukaguzi wa majengo. Hii itaondoa ujenzi holela.
    Unapouza kiwanja badala ya nyumba, kuna harmful ya rushwa.
    GSM walipata mwaka 2006, hawakujenga au hawajakiendeleza hadi 2017. Nielimisheni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Habari Mchanganyiko

Makonda autaka mgodi kubadilisha maisha ya wana-Geita

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ametoa wito kwa...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Je, miji ya Uingereza inafilisika?

Spread the loveMNAMO 1890, mwandishi mmoja wa habari Mmarekani aitwaye Julian Ralph...

error: Content is protected !!