May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rayvanny akiwasha Ufaransa, Mondi akizindua EP

Spread the love

MSANII wa Bongofleva kutoka lebo ya Wasafi, Raymond Mwakyusa ‘ Rayvanny’ amezidi kuzikwea ngazi za kimuziki duniani baada ya kuangusha bonge la shoo katika jiji la Paris nchini Ufaransa.Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)

Hayo yamejiri wakati bosi wake Naseeb Abdul ‘Diamond Platnums au Mondi’ akizindua EP yake inayokwenda kwa jina la FAO huku ikiwa na nyimbo kali 10.

Rayvanny ambaye pia ni mmiliki wa lebo ya Next Level Music jana tarehe 11 Machi, 2022 alipakia video akiwa kwenye jukwaa moja na gwiji wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Columbia, Maluma.

Rayvanny anaonekana na kusikika pia akimsifia Maluma kwa ueledi wake kwa lugha ya kimombo na kuwaacha midomo wazi wale wanaosema kwamba wasanii kutoka Afrika mashariki na hasusani Tanzania kuwa hawana uelewa wa kutosha katika lugha hiyo la Malkia wa Uingereza.

Mkali huyo wa ‘Tetema’ anasikika akiutaka umati kwenye ukumbi huo kumpigia makofi mara kumi nguli wa kibao cha ‘Hawai’, Maluma.

Watu wengi wamempongeza Rayvanny na kusema kwamba hiyo ni njia mojawapo ya kufika mbali kimuziki hasa katika teuzi za tuzo kubwa kama Grammy.

error: Content is protected !!