Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya GGML wafanya matembezi kuhamasisha mwezi wa afya ya akili
Afya

GGML wafanya matembezi kuhamasisha mwezi wa afya ya akili

Spread the love

WAKATI Tanzania ikiungana na dunia mwezi huu wa Oktoba kuadhimisha uhamasishaji wa afya ya akili, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Terry Strong ameongoza wafanyakazi na wakandarasi wa kampuni hiyo kufanya matembezi ya afya ndani ya eneo la mgodi huo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

GGML imechukua hatua hiyo muhimu katika kipindi hiki cha maadhimisho hayo ili kuikumbusha jamii umuhimu kufanya mazoezi kwa ustawi wa afya ya akili.

Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong akiwa pamoja na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo Vallence Ibrahim wakiongoza matembezi hayo ambayo yalishirikisha baadhi ya wafanyakazi na wakandarasa wa GGML

Wakiongozwa na Strong, zaidi ya wafanyakazi 30 wa GGML na wakandarasi walishiriki katika matembezi hayo yaliyochukua umbali wa kilomita 5 kuzunguka eneo la mgodi uliopo mkoani Geita.

Mkurugenzi huyo alisema matembezi hayo yalikuwa njia ya kuufurahisha na kuuchangamsha mwili, kuboresha mahusiano ya kijamii na ustawi wa kiakili miongoni mwa wafanyakazi na kukuza urafiki.

Aliongeza kuwa AngloGold Ashanti – GGML imekuwa ikizingatia kipaumbele cha ustawi wa kiafya kwa wafanyakazi wake.

Alisema “Mwezi huu, tunapofanya matembezi haya kuamsha ari mpya ya ufanyaji mazoezi mahali pa kazi, hii inadhihirisha kuwa ndani ya GGML kila mtu anathaminiwa, anajishughulisha na ana uwezo wa kiakili, tunajivunia kushiriki katika maadhimisho haya ya kimataifa na kuunga mkono ustawi wa afya ya akili kwa wafanyakazi wetu,” alisema na kuongeza;

“Afya ya akili inaathiri watu wengi; ni suala muhimu sana na nina furaha kuwa hapa kuliunga mkono kupitia maadhimisho haya. Ninawatakia nyinyi nyote na familia zenu heri na kuwatia moyo katika kuzingatia suala la kuangalia afya yako ya akili.

“GGML tunaamini kuwa wafanyakazi wenye afya bora na wanaojishughulisha ni muhimu kwa mafanikio yetu kama kampuni inayojishughulisha na uchimbaji madini. Tunathamini kila mfanyakazi aliye katika timu yetu na tumejitolea kuhakikisha anakuwa katika mazingira bora kwenye nyanja zote,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!