Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko GGML wadhamini mkutano mkuu wa wanajiolojia Arusha
Habari Mchanganyiko

GGML wadhamini mkutano mkuu wa wanajiolojia Arusha

Spread the love

Katika kuunga mkono ukuaji wa fani mbalimbali nchini, Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imejitosa kudhamini mkutano mkuu wa mwaka wa wanajiolojia wa Tanzania unaofanyika mkoani Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

 Mkutano huo ambao umeanza tarehe 4 Oktoba unatarajiwa kumalizika tarehe 7 Oktoba mwaka huu na unaratibiwa na Chama cha Watalaam wa Jiolojia Tanzania (TGS) kinachokadiriwa kuwa na wanachama zaidi ya 300.

 Akizungumza na Mwandishi wetu, Mrakibu wa Jiolojia katika Kampuni ya GGML, Eric Kalondwa alisema kampuni ya GGML imetoa shilingi milioni 25 za Kitanzania kudhamini mkutano huo uliofunguliwa na Waziri wa Madini, Dk. Dotto Biteko kwa niaba ya Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango lakini unatarajiwa kufungwa na Waziri wa Maji, Juma Aweso.

 Alisema katika mkutano huo ambao hufanyika kila mwaka kwenye mikoa tofauti tofauti, jumla ya wanajiolojia 11 kutoka mkoani Geita wameshiriki.

 Aliongeza kuwa mkutano huo umelenga kubadilishana uzoefu kwa sababu kuna progamu mbalimbali zinazolenga kuwaweka pamoja watu wenye fani zinazofanana.

Alisema wafanyakazi wa GGML ambao pia ni wana fani hiyo ya jiolojia, wamefaidika kwa namna mbalimbali tangu kianzishwe chama hicho.

Alisema mkutano wa mwaka huu unalenga kukazia suala la upatikanaji wa bodi ya wanajiolojia hasa ikizingatiwa fani hiyo inajumuisha watu kutoka maeneo mbalimbali ikiwamo wanaofanya kazi kwenye uchimbaji wa mafuta, kwenye maji, madini ya aina mbalimbali tofauti na na dhahabu.

Hata hivyo, alikiri kuwepo kwa changamoto ya uhaba wa wanawake kusomea fani hiyo, lakini akawatia shime wanawake kusomea fani ya jiolojia kwani haihitaji kuwa na nguvu kubwa ili kukidhi vigezo vya kuwa mwanajiolojia.

“GGML kwa kweli inafanya vizuri sana kuendeleza ma-jiolojia toka wanapokuja kujifunza kwa vitendo na wanaokuja kazini. Wale wanaopitia kwenye mgodi wetu hakika wanawasifia kwa mapokeo makubwa tunayowapatia kulingana na program ya mwaka ambayo huwa tunawaandalia,” alisema. 

Wanajiosayansi ni wataalam waliosomea na wenye uzoefu wa fani za jiolojia (miamba), jiofizikia, jiokemia, jioteknolojia na jiolojia ya mazingira na nyinginezo. 

Awali akifungua mkutano huo, Waziri wa madini Dk. Biteko alisema wizara iko katika hatua za mwisho  za kukamilisha mchakato wa kuanzishwa kwa  bodi ya wanajiolojia  na kuongeza kwamba, baada ya Serikali kukamilisha  sehemu yake,itatoa nafasi kwa  wadau  kutoa maoni kuhusu namna gani bodi hiyo iundwe, namna itakavyosimamiwa,  masuala yatakayohusisha vyanzo vya fedha na kuangalia masuala ya sheria.

Aliongeza kuwa, wakati Serikali inakamalimisha mchakato wa kuundwa kwa  bodi ya wanajiolojia   ni muhimu wajiolojia wakahakikisha wanaiendeleza taaluma ya jiolojia ili kuipatia nchi heshima ikiwemo  kuwawezesha wawezekaji kupata taarifa sahihi na hivyo kuvutia uwekezaji zaidi kwenye sekta ya Madini.

Pia aliwataka Wajiolojia nchini kuhakikisha wanaiheshimisha taaluma yao kwa kutoruhusu wasio waaminifu kuingilia majukumu ya kitaaluma kutokana na umuhimu wa shughuli za utafiti kwa maendeleo ya Sekta ya Madini na Taifa.

Aidha, Rais wa Chama cha Wataalam wajilojia Tanzania, Prof. Abdulkarim Mruma aliieleza hadhira kuhusu utajiri wa kijiolojia ambao nchi ya Tanzania imebarikiwa kuwa nao na kuelelezea namna bora ya kuitumia taaluma hiyo kwa maendeleo ya nchi na jamii nzima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!