Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Tangulizi NBAA kusherehekea siku ya uhasibu duniani, miaka 50 kuanzishwa kwake
Tangulizi

NBAA kusherehekea siku ya uhasibu duniani, miaka 50 kuanzishwa kwake

CPA, Maneno Pius Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA
Spread the love

BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA),  imeandaa maonesho ya huduma za kihasibu ikiwa sehemu ya shamra shamra za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Maonyesho hayo ya siku tatu yatakayofanyika mwezi Noveba tarehe 10 hadi 12 kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam yatahudhuriwa na mashirika na taasisi mbalimbali za uhasibu na ukaguzi.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA, Pius Maneno, wakati akizungumzia maonesho hayo yaliyobeba kauli mbiu ya ‘Utaalamu, Maslahi ya Umma na Uendelevu’

Alisema katika kuadhimisha miaka 50 bodi hiyo imeazimia kufanya shughuli mbalimbali za kusaidia jamii yakiwemo maonyesho hayo ya kihasibu ambapo watakaofika watapewa elimu ya uhasibu.

Alisema shughuli hizo za maadhimisho zilianza Agosti mwaka huu na zinatarajiwa kuhitikishwa tarehe 30 Novemba kwenye ukumbi wa APC Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Alisema lengo la maonesho hayo ni kuwaelimisha wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla jinsi ya kuandaa taarifa za hesabu za fedha, kodi na kuwasaidia kwenye Nyanja mbalimbali zinazohusu uhasibu na ukaguzi.

“Kwenye kniliki hiyo NBAA itaungana na wadau wake mbalimbali kama vile makampuni ya uhasibu na ukaguzi, Mamlaka ya Mapato TRA, Mamlaka ya Bima na mengine katika kutoa huduma hiyo,” alisema

Alisema katika miaka yake 50, NBAA imefanya mambo mengi makubwa ikiwemo kusajili wahasibu na wakaguzi na mpaka sasa waliofaulu mitihani ya bodi hiyo wanafikia 26,000 na kati ya hao, 12, 000 walifaulu katika ngazi ya CPA na 14,400 katika ngazi ya watunza vitabu vya hesabu.

“Pia tumesajili kampuni 450 za kutengeneza hesabu na ukaguzi haya ni maendeleo makubwa sana ndani ya miaka 50 ya NBAA, tumetunga viwango vya kutayarisha hesabu za fedha kwa sekta binafsi na kwa sekta ya umma” alisema

Aidha, alisema  wamefanikiwa kutengeneza kanuni za maadili ya wahasibu na wakaguzi na kuandaa semina na makongamano kila mwaka kitafa na kimataifa.

Alisema mwaka jana pekee NBAA ilifanikiwa kuandaa mikutanio zaidi ya 17 kwa wanachama wake pamoja na mashirika ikiwemo Benki Kuu Tanzania (BoT), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Alisema NBAA ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango yenye jukumu la kusimamia taaluma ya uhasibu na ukaguzi nchini iliyoanzishwa mwaka 1972.

Wakati huo huo, Mkurugenzi alisema siku ya tarehe 10 mwezi wa kumi na moja itakuwa siku ya kitamaifa ya kihasibu ambayo itafanyika kwenye hoteli ya Rotana jijini Dar des Salaam.

Alisema kwenye siku hiyo wataalamu mbalimbali wa fani hiyo watakusanyika na kufanya tathmini ya taaluma yao na kutoa mawazo mbalimbali ya namna ya kuendelea kuiboresha na kuendelea kusifika.

“NBAA inapenda kuwakaribisha wanataaluma wote wa fani ya uhasibu na ukaguzi siku hkiyo ya tarehe 10 mwezi wa kumi na moja katika hoteli ya Rotana kwani wataalamu watakutana na kubadilishana mawazo kuhusu taaluma yao na kiingilio itakuwa shilingi 100,000,” alisema CPA Pius Maneno

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!