Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Gari la Bobi Wine lashambuliwa kwa risasi
Kimataifa

Gari la Bobi Wine lashambuliwa kwa risasi

Bobi Wine
Spread the love

GARI la Robert Kyagulanyi ‘Bob Wine,’ mgombea urais nchini Uganda kupitia chama cha upinzani cha FDC, limeshambuliwa kwa risasi. Vinaripoti vyombo vya habari vya kimataifa … (endelea).

Hatua hiyo imesababisha Bobi Wine kusitisha kampeni zake huku maofisa wake kadhaa wakipigwa na kujeruhiwa nchini humo.

Akizungumzia tukio hilo lililotokea Kayunga, mashariki mwa Kampala, Bobi Wine amesema, risasi zilielekezwa kwenye gari lake ambapo zilitoboa matairi ya gari.

Katika sakata hilo, maofisa wanne wa Bobi Wine wamejeruhiwa huku video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikionesha mlipuko uliotokea umbali mchache toka pale alipokuwa.

Takriban wiki mbili zilizopita, watu 54 waliuawa wakati wafuasi wa mgombea huyo walipoandamana kudai aachiliwe huru baada ya kukamatwa na polisi katika mkutano wa kampeni.

Baadaye alishitakiwa kwa kukiuka masharti ya kukabiliana na janga la corona kwa kukusanya umati wa watu, lakini aliachiliwa kwa dhamana. Uchaguzi Mkuu nchini humo unatarajiwa kufanyika Januari 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!