November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC Dar aagiza usafi kila Jumamosi, Ma DC…

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Aboubakar Kunenge amewataka wakuu wa wilaya za jiji hilo (DC) kuhakikisha wanasimamia shughuli ya usafiri wa mazingira kila Jumamosi. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Kunenge amewataka wananchi wa Mkoa huo kuhakikisha kila Jumamosi kuanzia saa 12 hadi saa tatu asubuhi usafi unafanyika ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko na kuliweka jiji kuwa safi.

Mkuu hiyo wa mkoa, ametoa maagizo hayo jana Jumanne tarehe 1 Desemba 2020 wakati alipokuwa anazungumzia shughuli ya usafi inayotarajia kufanyika Jumamosi ya 5 Desemba.

Alisema Mkoa umejipanga vizuri kuhakikisha magari ya kubeba taka yanakuwa ya kutosha kwenye kila maeneo.

Aidha RC Kunenge aliwataka wakuu wa wilaya za Jiji hilo za Kinondoni, Ilala, Ubungo, Temeke na Kigamboni kuhakikisha wanasimamia usafi maeneo yao na kuhakikisha suala la usafi linazingatiwa na kila mmoja.

Pamoja na hayo RC Kunenge alitoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kuhakikisha suala la usafi linakuwa sehemu ya maisha yao na sio kusubiri kushurutishwa na sheria.

error: Content is protected !!