Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Michezo Fei Toto apeleka shangwe jangwani, kilio Kagera
Michezo

Fei Toto apeleka shangwe jangwani, kilio Kagera

Spread the love

 

BAO pekee lililofungwa dakika ya 24 na kiungo hodari wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ limetosha kupeleka shangwe kwa mashabiki wao ndani na nje ya Tanzania. Anaripoti Damas Ndembela, TUDARCo … (endelea).

Fei Toto alifunga bao hilo kwa shuti la mguu wa kushoto akiunganisha mpira uliotemwa ndani ya eneo la hatari na kipa wa Kagera Sugar, Ramadhan Mohamed.

Ni baada ya mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele kupiga shuti lililopanguliwa na Mohamed kisha kumkuta Fei Toto na kuukwamisha wavuni mpira huo.

Mchezo huo wa ligi kuu Tanzania Bara 2021/22, umepigwa leo Jumatano tarehe 29 Septemba 2021, katika Uwanja wa Kaitaba-Bukoba mkoani Kagera.

Yanga itashuka dimbani tena Jumamosi hii tarehe 2 Oktoba 2021 na Geita Gold katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Kocha wa Yanga, Mohamed Nabi akizungumza mara baada ya mchezo amesema, hatujaridhishwa na kiwango cha leo, kikubwa ni kupata alama tatu.”

Akitumia lugha ya Kifaransa huku kocha msaidizi Cedric Kaze akitafasiri kwa Kiswahili amesema wametoka kucheza na Simba ambayo walitumia nguvu nyingi na kuacha maua

Amesema, tumekosa magoli ya kutosha lakini kadri simu zinavyokwenda watafanya vizuri.

Kwa upande wake, Kocha wa Kagera Sugar, Francis Baraza wamecheza na timu kubwa na vijana wake wameonesha mchezo mzuri.

Baraza amesema, ligi ya msimu huu inaonesha ni ngumu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

Michezo

Beti na Meridianbet mechi za leo

Spread the love IKIWA leo hii ni Jumapili tulivu kabisa, Meridianbet wanamkwambia...

error: Content is protected !!