October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia akutana tena na Tony Blair

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu mstaafu wa Uingereza, Tony Blair. Anaripoti Wiston Josia, TUDARCo … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu imesema, mazungumzo hayo yamefanyika leo Jumatano, tarehe 29 Septemba 2021, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Tony Blair ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mabadiliko Ulimwenguni (Tony Blair Institute for Global Change) amemshukuru na kumhakikishia, Rais Samia kuwa taasisi yake inaunga mkono jitahada mbalimbali anazochukua katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.

Amesema ili kuwa na mafanikio ya haraka katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni muhimu kuwa na taarifa sahihi ambazo zitawezesha ufuatiliaji wa karibu wa miradi hiyo.

Kwa upande wake, Rais Samia amemshukuru, Tony Blair kwa kukutana nae na kumjulisha ufuatiliaji na uratibu wa masuala yanayofanywa na taasisi yake katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini Tanzania.

Aidha, Rais Samia amesema kwa sasa Serikali inaendelea na utekelezaji wa vipaumbele vyake kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.

Rais Samia amekutana na Tony Blair ikiwa ni takriban miezi miwili imepita tangu wawili hao walipokutana tarehe 22 Julai 2021, Ikulu jijini Dar es Salaam yaliyohusu masuala mbalimbali ikiwemo jinsi ya kukabiliana na janga laugonjwa wa corona (COVID-19).

Katika mazungumzo hayo ya awali, Blair alimhakikishia Rais Samia kuwa taasisi yake inaunga mkono jitahada mbalimbali anazochukua katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.

error: Content is protected !!