Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Jamhuri ilivyomhoji mke wa mshtakiwa kuhusu Mbowe
Habari za SiasaTangulizi

Jamhuri ilivyomhoji mke wa mshtakiwa kuhusu Mbowe

Spread the love

 

LILIAN Furaha Kibona, mke wa mshtakiwa wa pili, Adam Kasekwa, kwenye kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, amehojiwa na mawakili wa jamhuri kama aliwasiliana na Mbowe baada ya mume wake kutojulikana alipo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Lilian amehojiwa swali hilo leo Jumatano, tarehe 29 Septemba 2021, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam, mbele ya Jaji Mustapha Siyani.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Jenetreza Kitali, alimhoji Lilian wakati akitoa ushahidi wake aliieleza mahakama hiyo kama alimtafuta Mbowe kumueleza kuna watu walikwenda nyumbani kwake, Chalinze mkoani Pwani, kufanya upekuzi, ambaye alijibu akidai hakumtafuta.

Naye Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando, alimuuliza kama aliwahi kutoa taarifa katika serikali ya mtaa na polisi, kuhusu kupotea kwa mumewe, Kasekwa, ambaye amejibu akidai hakufanya hivyo.

Lilian alihojiwa maswali hayo, baada ya kudai mahakamani hapo kwamba, Askari Polisi wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi, Chalinze mkoani Pwani, walivunja mlango wa nyumba yake kisha wakafanya upekuzi na kuondoka na vitu ikiwemo begi la mumewe, kadi ya pikipiki na hati ya kiwanja.

Pia, Lilian alidai baada ya kutopata taarifa juu ya mahali alipo mumewe baada ya kuwasiliana naye mara ya mwisho simu, tarehe 5 Agosti 2021 akiwa Moshi mkoani Kilimanjaro, alimtafuta katika Hospitali na vituo vya Polisi, mkoani Dar es Salaam, alipopata taarifa kwamba amekamatwa na Polisi na kuletwa mkoani hapa.

Lilian alidai, mume wake aliyekuwa Komandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kabla ya kuondoka nyumbani kwake, alimueleza anakwenda Moshi mkoani Kilimanjaro, kufanya kazi ya kumlinda Mbowe.

Kesi hiyo ndogo ya imetokana na mapingamizi ya utetezi, kupinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili katika kesi ya msingi, Adam Kasekwa yasitumike mahaiamani hapo kama ushahidi, ukidai yalichukuliwa kinyume cha sheria.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 19 Oktoba 2021, ambapo mahakama hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi wa kesi hiyo ndogo, baada ya pande zote mbili kufunga ushahidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

error: Content is protected !!