Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Fatma Karume ampa ‘dawa’ JPM
Tangulizi

Fatma Karume ampa ‘dawa’ JPM

Spread the love

FATMA Karume, mwanasheria wa Mahakama Kuu na Rais Mstaafu wa Chama cha Wanasheria nchini (TLS) amesema, ili mahakama ziwe huru, watendaji wake hawapaswi kuteuliwa na muhimili mwingine. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

“Ili mahakama iwe huru, haitoshi tu kutamkwa kwenye Katiba kuwa kuna Mahakama Huru, lazima kuwe na muundo huru wa kiutendaji.

“Kwenye muundo huo, lazima utizame uteuzi wa majaji. Inavyojiendesha kifedha. Huwezi kuita Mahakama Huru wakati uteuzi wa majaji unafanywa na mhimili mwingine,” amesema Fatma alipozungumza na MwanaHALISI Online tarehe 6 Januari 2020, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujbu wa mwanasheria huyo, ili mhimili wa mahakama uwe huru, unatakiwa kujitegemea kifedha.

“Bajeti ya mahakama inategemea serikali. Miundo mingi dunia mahakama lazima iwe huru kuunda bajeti yake. Isiingiliwe na serikali.

“Inawezekanaje mhimili wa haki ipewe bil 120? Mahakama ina mahakimu 2,000, ina majengo lazima ijenge ina majaji zaidi ya 60, lazima iwe na magari, ilipe umeme, inunue makaratasi.

“Huwezi kuendesha mahakama kama hivi. Haiwezekani majaji wakateuliwa na mtu mmoja. Haiwezekani,” amesisitiza Fatma.

Pia amesema, kinacho kwanza utoaji haki kwenye Mahakama za Tanzania ni kushindwa kutatuliwa mifumo kufikia haki hiyo.

Amesema, Rais John Magufuli anapaswa kubadili mifumo inayochelewesha haki ili kumaliza tatizo hilo, sambamba na kupunguza mlundikano wa mahabusu.

“Huwezi kutatua tatizo la mlundikano wa watu mahabusu kama hujui msingi wa tatizo. Kuna sababu nyingi, moja kesi zenyewe zinakwenda mahakamani kabla ya upelelezi kukamilika.

“Kesi zinaahirishwa mara kwa mara, ukosefu wa pesa za kuendesha kesi. Kama sababu hizo hazitaondolewa, tatizo hilo haliwezi kuisha,” amesema Fatma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

error: Content is protected !!