April 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wanne kizimbani kwa kuiibia polisi Sh 798 milioni

Spread the love

WATU Wanne akiwamo Ofisa wa Jeshi la Polisi, wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa makosa ya kuiingizia hasara jeshi hilo na utakatishaji wa fedha kiasi cha Sh 798 milioni. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Leo tarehe 6 Januari 2020 , Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Salum Ali, amesomea mashtaka matatu watuhumiwa hao ambao  ni Emmanuel Mkilia (44), Ofisa wa Polisi; Dolnald Mhaiki (39) mfanyabiashara; Abdi Ally (48), mfanyabiashara na Mohyadini Hussein (56) mfanyabiashara.

Wankyo amewasomea shtaka la kwanza la kuliingizia hasara Jeshi la Polisi kiasi cha Sh 798,789,272.

Shtaka la Pili ni kujiingizia pesa kwa njia ya udanganyifu ambao inadaiwa kutendwa na washtakiwa wote kati ya tarehe 19 Machi 2013 na tarehe 18 Oktoba 2013, ambapo watuhumiwa walidanganya kuwa wamefunga mfumo wa  kitaalamu wa taarifa za washukiwa kwenye vituo vine vya polisi jambo ambalo sio kweli.

Shtaka la mwisho ni utakatishaji fedha haramu ambapo watuhumiwa wote wanadaiwa kutakatisha kiasi cha Shilingi  798,789,272.

error: Content is protected !!