April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kizimbani kwa kukeketa watoto wake

Spread the love

COSMAS Chacha (45), Mkazi wa Kivule, jijini Dar es Salaam amefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa makosa ya ukeketeji watoto wake watatu. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Akisoma mashtaka hayo leo tarehe 6 Januari 2020 Wakili Serikali, Faraji Nguka mbele ya  Hakimu Rashid Chaungu, amedai kuwa tarehe 8 Desemba  2019, katika eneo la kivule jijini Dar es Salaam, mshtkiwa ambaye ni baba mzazi wa watoto hao walio chini ya umri wa miaka 18 na mwenye jukumu la kuwalea, aliwapeleka kukeketwa na kuwasababishia maumivu makali.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mtuhumiwa alikana kutenda makosa hayo na upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Hakimu Chaungu alitoa masharti ya dhamana ya Sh. 5 milioni kwa wadhamini wawili, lakini mshtakiwa hajatimiza masharti ya dhamana kwa mmoja kukosa utambulisho na barua kutopitia kwa mkurugenzi hivyo amerejeshwa rumande.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 20 Januari 2020.

error: Content is protected !!