April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Tito: Utetezi waja na rai mpya kwa serikali

Spread the love

UPANDE wa utetezi kwenye kesi namba 137/2019, inawamkabili wanaharakati Tito Magoti na Theodory Giyan, umetoa rai kwa serikali kutokamata watuhumiwa bila kufanya upelelezi. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Rai hiyo imetolewa leo tarehe 7 Januari 2020, kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega.

Fluguence Masawe, wakili wa utetezi ametoa rai hiyo baada ya wakili wa serikali, Renatus Mkude kuieleza mahakama kwamba upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.

Hoja ya wakili Masawe imeungwa mkono na wakili Anna Henga ambaye ni Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binaadam (LHRC), ambaye amesisitiza kuwa serikali haikutakiwa kumkamata na kumshitaka Tito na Giyan kabla ya kufanya upelelezi.

Jopo la mawakili saba wa utetezi kutoka LHRC na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC, wamesisitiza kuharakishwa upelelezi wa shauri hilo.

Hakimu Mtega ameahiirisha shauri hilo mpaka tarehe 21 Januri 2020.

Awali tarehe 24 Desemba 2019, Tito na Giyan ambao ni maofisa wa LHRC, walifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashtaka matatu ambayo ni kushiriki genge la uhalifu, kumiliki program ya Kompyuta kwa lengo la kufanya uhalifu na kutakatisha fedha kiasi cha Sh.17 milioni.

error: Content is protected !!