Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Familia ya Lowassa yafunguka, yamtaja Rais Samia
Habari za SiasaTangulizi

Familia ya Lowassa yafunguka, yamtaja Rais Samia

Spread the love

FAMILIA ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Lowassa, imesema kiongozi huyo mstaafu alipigania uhai wake kabla ya mauti kumkuta. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumanne na Msemaji wa Familia ya Lowassa, Fredy Lowassa katika shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa mwanasiasa huyo aliyefariki dunia tarehe 10 Februari mwaka huu.

“Baba alipata umauti siku ya Jumamosi lakini kwa kweli tunasema tumelipokea hili kwa moyo wa imani kwasababu baba aligua muda mrefu, kama mlivyosema baba ni mpambanaji, kweli alipambana sana mpaka dakika ya mwisho lakini tunamshukuru Mungu na familia tumepokea kwa amani tunasema akapumzike kwa amani,” amesema Fredy.

“Kipekee naomba kutoa shukrani za familia kwa Rais Samia ukweli kama isingekuwa Rais Samia baba yetu asingefika hata hiyo Jumamosi. Mama Samia amekuwa ndugu, mlezi na mama mzazi kwetu kwa kweli hatuna cha kumlipa tunamshukuru sana. Siku anaondoka kuelekea Italia tayari hali ya baba ilikuwa imebadilika lakini alimtuma mkuu wa majeshi akawa anampa update kila baada ya nusu saa mpaka umauti unamkuta saa nane mchana,” amesema Fredy.

Amesema msiba huo sio wa ukoo wa Lowassa peke yake, bali wa taifa zima hasa wazazi na walezi ambao watoto wao wamesoma shule za sekondari za kata ambazo enzi za uhai wake akiwa Waziri Mkuu, Lowassa alisimamia ujenzi wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!