Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM: Tumejifunza kwa Lowassa
Habari za SiasaTangulizi

CCM: Tumejifunza kwa Lowassa

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema yapo baadhi ya masuala kimejifunza kutoka kwa aliyekuwa kada wake na waziri Mkuu mstaafu, Hayati Edward Lowassa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam …(endelea).

Hayo yamebainishwa leo Jumanne na Naibu Katibu Mkuu-Bara mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Anamringi Macha katika shughuli ya kuuaga mwili wa Lowassa, aliyefariki dunia tarehe 10 Februari 2024.

Naibu Katibu Mkuu-Bara mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Anamringi Macha.

“Baada ya kupata taarifa ya msiba naamini wote mtakubaliana kwamba historia ya mpendwa wetu ilianza kurejewa na viongozi na wananchi kupitia vyombo vya habari, historia yake kuhusu wema alioutenda kwa ajili ya taifa letu tuseme yote tumeyasikia na tunachokiomba kila mmoja kuona kipi akirejee kwa ajili ya kuendelea kujenga taifa letu,” amesema Macha na kuongeza:

“Sehemu kubwa ya maisha yake lazima tukubali alikuwa katika familia ya CCM na sisi tukiri kwamba yapo tuliyojifunza kwake na yapo ambayo ni rejea yataendelea kuimarisha chama chetu na siasa ya nchi yetu kwa ujumla.”

Miongoni mwa historia ya Lowassa ambayo haitafutika katika siasa za Tanzania, ni uamuzi wake wa kujiunga na upinzani (Chadema), kisha kugombea urais wa Tanzania  baada ya CCM kushindwa kumpa nafasi hiyo.

Lowassa aligombea urais wa Tanzania 2015 kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya kushindwa miaka michache baadae alirejea CCM.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!