May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Emirates wamfuta jasho msemaji Simba, wamzawadia Mil 2

Spread the love

 

Kampuni ya Emirates Aluminium Profile imemzawadia kiasi cha shilingi Milioni mbili, Meneja Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally, kwa kutambua mchango wake ndani ya klabu hiyo katika siku za hivi karibuni. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Hii leo tarehe 7 Mei 2022 mbele ya wanahabari, msemaji huyo,alikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya milioni mbili na Afisa Mahusiano wa kampuni hiyo Issa Maeda ambao pia utoa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa klabu hiyo.

Akizungumza wakati akimkabidhi hundi hiyo, Maeda alisema kuwa tuzo hiyo ni binafsi kutoka Emirates na haina mchakato wa kupigiwa kura ba kampuni imeona impatie kutokana kufanya kazi kubwa.

“Hii ni tuzo maalumu kwa mwezi wanne na haina mchakato wa kupiga kura bali hii ni tuzo binfasi kwa kampuni ya Emirates na Ahmed Ally maana aliupiga mwingi.” Alisema Maeda

Katika kipindi cha hivi karibuni. Ahmed alifanikiwa kuhamamisha mashabiki wa klabu hiyo na kufanikiwa kujitokeza kwa wingi katika michezo ya kimataifa ya kombe l;a shirikisho Barani Afrika walipokuwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Ahmed alisema kuwa hakutarajia kukutana na kitu kama hiko, kwa jambo lilompeleka kwenye ofisi za kampuni hiyo ni kwenye shughuli ya kumkabidhi tuzo ya mwezi mchezaji Henock Inonga.

“Niwashukuru Emirates kwa zawadi hii kubwa, hawakumwambia mtu lakini nilkuja hapa kumleta Ingona na mimi nikajikuta nina tuzo yangu, mzigo ni mzito milioni mbili sio kazi ndogo, jimefarijika sana.”

Kwenye michezo yote hiyo ambao Simba walikuwa nyumbani kwenye hatua ya makundi, walifanikiwa kuondoka na pointi tisa na kushinda mchezo wa mzunguko wa kwanza war obo fainali dhidi ya Orlando uliochezwa kwenye dimba hilo.

error: Content is protected !!