May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Inonga akabadhiwa Tuzo na Emirates mchezaji bora Aprili

Spread the love

 

Mlinzi wa kati wa klabu ya Simba, Henock Inonga amekabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mashabiki (Emirate Aluminium Simba ACP Fans Player of the Month) kwa mwezi Aprili 2022, mara baada ya kuwashinda Shomary Kapombe na Josh Onyango. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea.

Mchezaji huyo amekabidhiwa tuzo hiyo hii leo tarehe 7 Mei 2022, kwenye makao makuu makuu ya kampuni ya Emirates Aluminiun Sinza jijini Dar es Salaam.

Beki huyo ambaye amekuwa na kiwango bora hivi karibuni aliibuka kidedea mara baada ya kupata kura 2277 sawa na asilimia 82.14, huku akifuatiwa na Kapombe aliyepata kura 457 sawa na asilimia 16.49 na wa mwisho ni Onyango aliyepata kura 38 sawa na asilimia 1.37.

Ndani ya mwezi Aprili, Inonga amecheza mechi nne sawa na dakika 360 huku akionyesha kiwango safi kwenye michezo yote.

error: Content is protected !!