Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Michezo Kauli ya udhaifu wa Ligi yamuibua Ally Mayay
Michezo

Kauli ya udhaifu wa Ligi yamuibua Ally Mayay

Spread the love

 

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga, Ally Mayay amefunga juu ya ubora wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kusema kuwa wanaosema kuwa Ligi hiyo ni dhaifu wanalinganisha na Ligi ipi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mjadala wa ubora wa Ligi hiyo umeibuka hivi karibuni, kufuatia msemaji wa klabu ya Simba Ahmed Ally, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, kwa kuandika kuwa, Ligi ya msimu ina timu nyingi ambazo ni dhaifu hivyo bingwa anaweza kupatikana kwa kuwafunga wadhaifu.

“Timu nyingi Msimu huu zimekua dhaifu, tupo mzunguko wa 22 lakin ni timu tatu tu zimefikisha point 30, Msimu uliopita hadi kufika mzunguko wa 22, japo timu zilikua nyingi lakini timu 7 zilikua na points 30. Hii ni hatari kwa sababu Bingwa anaweza kupatikana kwa kufunga waidhaifu wengi.” Aliandika Ahmed

Taarifa hiyo ilipelekea kumtafuta mkongwe wa soka nchini ambae pia ni mchambuzi, Ally Mayay (Tembele) na kufafanua kuwa, kama Ligi yetu utataka kuifananisha na Ligi za barani Ulaya au Afrika ya Kaskazini basi lazima utaiona dhaifu, lakini kwa ukanda huu wa Afrika mashariki ni moja ya Ligi Bora.

“Lazima kwanza ujue unajilinganisha na nani, kama unalinganisha na timu za ulaya ni kweli dhaifu, na hata Afrika Kaskazini ni miongozni mwa Ligi zilizokuwa kwenye viwango bora.”

“Hatuwezi kusema dhaifu kwa ukanda wa Afrika Mashariki, sisi tupo juu ukiacha sudani kwa kuwa bado baadhi ya timu zao zinafanya vizuri.” Alisema mchambuzi huyo

Mpaka sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imebakisha michezo nane kwa baadhi ya timu, huku klabu ya Yanga ikiwa kwenye kilele cha usukani wakiwa na  56, huku wakifutiwa na Simba kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 43.

2 Comments

  • Ni kweli ligi ni dhaifu.
    Time zetu hazifiki nusu fainali ya Afrika. Migogoro ni udhaifu pia.
    Hazitoi wachezaji Ulaya. Pia, wengi ni wachezaji wa kigeni.
    Hata Mbwana Samatta alishindwa kufurukuta kule Premier League.
    Wako wapi wenye umri wa miaka 17, 18, 19, 20, na 21 wanaochezea time zetu kubwa. Huo ni udhaifu kwa sababu uzoefu unashinda ufundi!
    Ufundi wa soka ukitawala, basi mpira siyo dhaifu. Ligi daraja la pili ni rafu na fujo tupu. Huu pia ni udhaifu.

  • Ligi ya nbc na tmu zake sio dhaifu na nimegundua watu wengi hawafikrii
    Tmu za tanzania ukitoa timu ya yanga zilzobaki zinapambania nafas ya uwakilish wa nch kimataifa ambayo ni nafasi ya 2,3,na ya 4 hazichez kushuka daraja. Kwani ukitaka kushuka daraja si unakubali kupoteza? Sasa kuna tmu ya namna hyo mwaka huu?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!