Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mwinyi aungana na Samia kuuaga mwili wa baba yake
Habari za Siasa

Dk. Mwinyi aungana na Samia kuuaga mwili wa baba yake

Spread the love

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na wananchi, viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mzee Ali Hassan Mwinyi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Shughuli za kuaga mwili wa Mzee Mwinyi zimefanyika katika Uwanja  wa Amaan, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo tarehe 2 Machi 2024.

Pia Rais Samia ameongoza viongozi mbalimbali kutoa salamu za rambirambi  na pole kwa watanzania na familia ya Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na kutoa heshima za mwisho kwa Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi katika uwanja huo.

Viongozi mbalimbali wameshiriki wakiwemo wa Serikali ya  SMT na SMZ,  wa Vyama vya siasa, Vyombo vya ulinzi na usalama, Dini, Waheshimiwa Mabalozi pia wawakilishi wa nje ya Tanzania wakiwemo  Namibia, Burundi na Comoro walitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Nchi zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!