NAIBU Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dk. Festo Dugange leo Jumanne ameonekana kwa mara ya kwanza hadharani kwenye shughuli ya kiserikali ikiwa imepita miezi miwili na ushee tangu alipopata ajali tarehe 26 Aprili 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Dk. Dugange awali aliripotiwa kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma baada ya kupata ajali hiyo iliyozua maswali mengi na kuhusishwa na kifo cha mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).
Ajali hiyo ilitokea katika barabara ya Iyumbu, maeneo ya St. Peter Clever ikihusisha gari namba T454 DWV aina ya Toyota Land Cruiser iliyokuwa ikiendeshwa na Dk. Dugange.
Hata hivyo, leo tarehe 25 Julai 2023 ameonekana akisalimiana na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (katikati) pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde (kushoto) katika Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa katika Uwanja wa Mpya wa Mashujaa eneo la Mji wa Serikali – Mtumba, Dodoma.
Mgeni rasmi ni Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi.
Leave a comment