Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Biteko aacha alama sekta ya madini
Habari Mchanganyiko

Dk. Biteko aacha alama sekta ya madini

Spread the love

Dk. Biteko aacha alama sekta ya madini

Imeelezwa kuwa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk.  Doto Biteko ameacha alama kubwa katika Sekta ya Madini katika kipindi chote alichokuwa Waziri wa Madini na kupelekea mabadiliko makubwa katika sekta hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 23 Septemba 2023 na Viongozi mbalimbali wa Serikali na wadau wa sekta ya madini wakati Dk. Biteko akifungua rasmi Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini katika viwanja vya EPZ Bombambili Mkoani Geita.

 

Antony Mavunde

Akizungumza baada ya salaam hizo Dk. Biteko amesema kuwa masuala yote yaliyozungumzwa na mafanikio hayo katika Sekta ya Madini yametokana usimamizi madhubuti wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye sekta hiyo.

Kuhusu Waziri wa Madini Anthony Mavunde amemtaka afanye kazi kwa bidii na kuwataka wadau wa Sekta ya Madini nchini kumuunga mkono katika utekelezaji wa majukumu yake kila siku.

“Vision 2030, Madini Maisha na Utajiri itachangia kuleta mabadiliko na kupunguza umaskini kwa wananchi wengi nchini, Sekta hii ni moyo wa uchumi wa nchi tuitumie kikamilifu ili kuleta mabadiliko,” amesema Dkt. Biteko.

Aidha, ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa kununua kilo 400 za dhahabu zilizosafiswa katika viwanda vya ndani vya kuchenjua dhahabu nchini. Ameitaka Benki Kuu kuwaunga mkono wachimbaji wa madini nchini ili kuleta tija na kuongeza mchango wa Sekta ya Madini.

Kwa upande, wake Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema kuwa Dkt. Biteko ameifanya Sekta ya Madini imekua Sekta Kiongozi kwenye uchumi wa Nchi. Aidha ameipongeza mkoa wa Geita kwa kuandaa maonesho hayo kuwa yenye tija kwa wananchi wa mkoa wa Geita.

” Nimekuja na Vision 2030, Madini ni Maisha na Utajiri ili hadi kufikia mwaka huo tuwe tumefanya tafiti katika eneo lote la nchi ya Tanzania ili wananchi wa waweze kunufaika na rasilimali madini,” amesema Waziri Mavunde.

Pia, amesema ifikapo mwezi Oktoba Serikali itakabidhi mashine tano za uchorongaji wa Madini ili ziwe msaada kwa wachimbaji wadogo wa madini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela amesema maonesho hayo yamefungua fursa za uwekezaji kwa wananchi wanaozunguka maeneo mbalimbali mkoani Geita kwa kubadilisha maisha ya jamii hiyo.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Geita Constantine Kanyasu amesema kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk. Biteko ameacha alama kubwa katika Sekta ya Madini nchini. Aidha , ameongeza kuwa  mchango wake utakumbukwa katika nyanja zote hususan katika kuwaendeleza wachimbaji wadogo na kuwawekea mazingira rafiki ya uchimbaji na uwekezaji.

Wengine walioshiriki katika ufunguzi huo ni Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa, Wabunge, Viongozi wa Vyama vya siasa,  Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali, Wakuu wa Taasisi za Umma na wadau mbalimbali wa sekta  ya madini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!