Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko DED Ujiji azindua redio mpya Kigoma, awang’ata sikio vijana
Habari Mchanganyiko

DED Ujiji azindua redio mpya Kigoma, awang’ata sikio vijana

Spread the love

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mwantum Mgonja ameipongeza kampuni ya Mainstream Media Limited kwa uwekezaji uliofanywa katika mkoa wa Kigoma.  Anaripoti Mwandishi Wetu…(endekea).

Mkurugenzi huyo ametoa pongezi hizo leo tarehe 10 Julai 2023 katika mahojiano katika studio za Main Fm kwenye tukio la kuwasha kipaza sauti (mic) kwa mara ya kwanza.

Ni baada ya kampuni hiyo  kuanzisha kituo che redio cha Main Fm 91.7 ambacho kimelenga kutoa habari na taarifa katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo yanayofanywa  ndani ya mkoa wa Kigoma.

Mkurugenzi huyo amesema serikali imetoa fedha kwa ajili ya kujenga na kuboresha miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya manispaa ya Kigoma Ujiji.

Amesema miradi hiyo inagusa sekta mbalimbali hususani afya na elimu.

Ameongeza kuwa redio hiyo itasaidia kutoa taarifa za aina hiyo kwa umma huku akishukuru kwa kupata fursa ya kuwa wa kwanza  kukizindua kituo hicho.

Aidha, mkurugenzi huyo akizungumza mambo mbalimbali yanayohusu wilaya hiyo, amefafanua kuwa mfuko wa maendeleo ya vijana unafanyiwa marekebisho hivyo vijana wa mkoa wa Kigoma waendelee kusikiliza vyombo vya habari hususani Main fm 91.7 kwa ajili ya kujua fursa hizo zinazopatikana ndani ya mkoa wa Kigoma.

Ametaja fursa hizo kuwa ni pamoja mikopo nafuu inayotolewa na serikali kwa ajili ya kuwainua vijana kiuchumi.

Mwantum alikuwa ameambatana na diwani viti maalum kata ya Mwanga Kusini, mtendaji wa kata ya Mwanga Kusini na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa kilimahewa pamoja na wadau mbalimbali kutoka  ndani ya mkoa wa  Kigoma.

Mainstream Media Limited, pamoja na uwekezaji huo pia wametoa fursa za ajira kwa watangazaji na wadau wa tasnia ya habari kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuhakikisha kuwa kituo chao hicho kinafikisha ujumbe kwa urahisi na haraka zaidi kote duniani.

Zoezi la kuwasha vipaaza sauti (Mic) lilienda sambamba na kuwaruhusu wasikilizaji wa redio hii duniani kote kuisikiliza kupitia kwenye masafa ya 91.7 FM Kigoma na kupitia kwenye tovuti ya Main FM.

Pia Meneja wa kituo Felician Hulilo, amesema kuwa Main FM imeanzia Kigoma lakini menejimenti yake imelenga kuipeleka redio hii katika mikoa yote ya Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!