MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni amewataka watendaji Serikali kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ya maji, ili iweze kukamilika kwa wakati. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Alisema pamoja na fedha za mradi kupelekwa mradi huo haujaanza kufanya kazi hali ambayo imelete malalamiko kwa wananchi.
Mgeni aliwataka watendaji wote wanaohusika kuhakikisha mradi huo unakamilika ili kuondoa tatizo la maji kwa wananchi.
DC Mgeni alimtaka Meneja RUWASA Wilaya ya Same kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati, ili wananchi wapate huduma za maji.
Pia amewataka kunapotokea mabadiliko yoyote katika sekta ya maji ikiwemo kupanda kwa bili za maji kutoka Sh. 2000 hadi 5000 kwa mwezi ambayo pia wananchi hawakuwa na uelewa kuhusiana na ongezeko hilo.
“Ni vema kutumia vikao vya kisheria vya bodi ya maji kutoa ufafanuzi kwa wananchi badala ya kunyamaza na kuzua masuala mengi toka kwa wananchi,”alisema.
Wananchi walimweleza DC kuwa Waziri wa Maji Juma Awezo, aliagiza hapo Julai 2021 ukarabati ufanyike ndani ya miezi mitatu uwe umekamilika ili wananchi waweze kupata huduma ya maji, lakini mpaka sasa hawajui kinachoendelea kwani tatizo la maji liko palepale na kwamba hawajui mradi huo umekamilika.
Leave a comment