Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Daraja jipya la Wami laanza kutumika
Habari MchanganyikoTangulizi

Daraja jipya la Wami laanza kutumika

Daraja la mto Wami
Spread the love

 

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa ameruhusu Magari kuanza kutumia daraja jipya la wami kufuatia Ujenzi wake kukamilika kwa asilimia 96. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani … (endelea).

Kaizungumza leo Alhamis tarehe 27 Oktoba, 2022 mara baada ya kukagua daraja hilo, Profesa Mbarawa amewataka viongozi na wananchi wa mkoa wa Pwani, kuhakikisha daraja hilo lenye urefu wa mita 513.5 na upana mita 11.85 linalindwa ili kudumu kwa zaidi ya miaka 120 iliyokusudiwa kutumika.

“Daraja limekamilika kwa asilimia 96 hivyo madereva na watumiaji wa daraja hili, tumieni kwa uangalifu na kulitunza kwa kuwa kazi ndogo ndogo za ukamilishaji zinaendelea,” amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, Prof. Mbarawa amewataka viongozi kutoa ushirikiano kwa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na wakandarasi wanaojenga barabara ya magari yaendayo haraka ya Kibaha-Chalinze-Morogoro Express Way (km 215)Ili kuwezesha ujenzi kuanza kwa wakati.

“Serikali inaendelea kuufungua mkoa wa Pwani kwa kuendeleza Ujenzi wa barabara kutoka Pangani-Horohoro-Lungalunga- hadi Mombasa nchini Kenya ambayo itaboresha uchumi wa viwanda na kukuza utalii katika eneo hilo la kimkakati,” ameongezea Profesa Mbarawa.

Kwa Upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Dorothy Mtenga, amesema zaidi ya Sh 75 bilioni zimetumika katika ujenzi wa daraja hilo lilokusudiwa kutatua changamoto za daraja la mwanzo ambalo lilikuwa halikidhi mahitaji ya magari yanayopita kwa kuwa lilijengwa miaka 63 iliyopita na lilikuwa na njia moja.

Naye Mkuu wa Wiaya ya Bagamoyo, Zainabu Abdalah Issa, ameishukuru Serikali hususani Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa utekeleza wa miradi ya miundombinu ya kimkakati katika Mkoa wa Pwani, inayochochea maendeleo ya Viwanda, Utalii na Biashara.

Aidha, amemhakikishia Waziri Mbarawa, kuwa madaraja na barabara zinazojengwa katika mkoa wa Pwani, zitatunzwa vizuri.

Daraja la mto Wami

Kwa upande wake Mbunge wa Chalinze ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete, ameishukuru Serikali kwa kuendeleza miradi ya miundombinu katika mkoa wa Pwani ili kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo.

Daraja jipya la Wami, linaunganisha mkoa wa Pwani na Tanga, litachochea ustawi wa jamii kiuchumi na kuleta maendeleo kwa mikoa ya kaskazini mwa Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

error: Content is protected !!