MWENYEKITI wa Chama cha Ukombuzi wa Umma (Chauuma), Hashimu Rungwe amemshauri Rais Samia Suluhu Hassan kuzifuta sheria zote kandamizi kwa vyombo vya habari kwa kuwa sheria hizo zikwamisha uhuru wa habari. Anaripoti Faki, Dar es Salaam … (endelea).
Akizingumza na MwanaHALISI Online Rungwe leo tarehe 27 Oktoba, 2022 amesema kuwa Rais Samia anamamlaka ya kuondoa sheria hizo kwa kuwa zinakwamisha maendeleo ya nchi.
“Siku za nyuma mbona waandishi mlikuwepo mlisababisha matatizo gani?
“Mimi nafikiri Rais angeangalia hizi sheria rundo hovyo zilizowaandama waandishi kwa sababu juzi tu kulikuwa na kijana tunamtetea alikuwa anashtakiwa kwa sheria hizo. Akina Tundu Lissu nao walishtakiwa kwa sheria ya magazeti” amesema Rungwe.
Rungwe ambaye pia ni mbobevu wa masuala ya sheria amemuomba Rais Samia afanye mabadiliko yatakatoleta nafuu kwa waandishi wa habari na wanasiasa wahanga wa sheria kandamizi.
“Tunamuomba Rais Samia uwaachiwe hawa waandishi na hawa waliofungwa kwa sababu za kisiasa wawe huru nchi inawahitaji” amesema.
Rungwe amesema kukwepa kuvipa uhuru vyombo vya habari ni kuvunja katiba kwa kuwa suala hilo lipo wazi kuwa ni haki ya wananchi
“Vyombo vya habari kuwa huru ni suala la kikatiba hilo suala linaeleweka kuwa wananchi wanataka kupata habari wawelekee wananchi wenzao ili wananchi waelewe kinachoendelea nchini.
Leave a comment