TANZANIA imekuwa mwenyeji wa mashindano ya dunia ya utanashati, urembo na mtindo ya watu wenye tatizo la kusikia ‘viziwi’ (Miss & Mister Deaf). Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Mashindano hayo yanatarajia kufanyika tarehe 29 hadi 31 Oktoba mwaka huu katika Ukumbi wa kimataifa wa Mwl Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Serikali ya Tanzania imesema kuwa inachukulia mashindano hayo kama fursa ya kuitangaza nchi.
Dk. Emmanuel Ishongoma Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka kwenye Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Wasanii amesema mashindano hayo yatatumiwa kuitangaza nchi.
“Kama mnavyofahamu shughuli hii tunaifanya lakini sisi wenyewe kama nchi tunamkakati wetu wa kuitangaza nchi kimataifa na hii ni sehemu ya mkakati huo na baada ya hapa tunampango wa kwenda Ngorongoro, Zanzibar, na Serengeti ” alisema Dk. Ishongoma.
Kwa upande washiriki wa Tanzania amesema tayari wamejianda vya kutosha kwa ajili ya kutwaa ushindi wa mataji hayo.
Primrose Madhiba mshiriki wa mashindano hayo kutoka Zimbabwe amesema kuwa amefurahi kufika Tanzania na amejianda kushindana kwa ajili ya kupeperusha bendera ya taifa lake.
Habibu Mrope Mwenyekiti wa Viziwa Afrika amesema mashindano hayo yatashirikisha washiriki 200. kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Leave a comment