TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imetoa fursa kwa wanafunzi wabunifu kujiunga na Kumbi mama ya bunifu Buni Hub ambayo inaendesha programu mbalimbali za ubunifu kwa lengo la kuendeleza na kukuza vipaji. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Akizungumza Jumapili tarehe 20 Machi 2022, na washiriki wa mashindano ya ubunifu ya Teensinai Mkurugenzi wa Ubunifu na Teknolojia wa COSTECH, Dk. Gerald Kafuku amesema kuwa Tanzania imebeba hazina ya vipaji ambayo COSTECH inavigundua na kuvikuza na kwamba hazina hiyo inakwenda kuwa mlango wa mafanikio kwenye maendeleo ya Teknolojia nchini.
Mchuano huo ulidhaminiwa na Ubalozi wa Marekani nchini, na Smile Communication iliwashirikisha wabunifu wanafunzi waliotoka kwenye shule mbalimbali nchini.
Amesema COSTECH inakwenda sambamba na sera za maendeleo ya Taifa na kwamba Tume hiyo ina lengo la kuhakikisha wataalam wa Teknolojia hawatoki nje ya nchi.
Amefafanua kuwa COSTECH imeanzisha kumbi mama ya bunifu Buni Hub kwa lengo la kuwakuza wabunifu kama ambavyo tayari wabunifu wengine wamepaa kimataifa kupitia mpango huo.
“Hapa kwetu tumeanzisha mpango wa Buni kwa ajili ya vijana hawa wabunifu, na hapa tulishatengeneza vijana ambao ni mamilionea kwa sasa kutokana na COSTECH kuwapa mtaji, kuwaendeleza na kuwashika mikono.
“Tunawakaribisha wabunifu wote kuanzia sasa wajiandikishe hapa Buni ili tuwasaidie kwenye ubunifu wao wa kiteknolojia.
Rose Mariki mmoja wa majaji wa mashindano hayo ameipongeza COSTECH kwa kuendeleza vipaji vya ubunifu ambavyo Taifa litapiga hatua kwenye ubunifu huo.
Suleiman Abdallah Mshiriki wa mashindano hayo amesema kuwa shindano hilo limempa ujasiri na matumaini ya kukuza kipaji chake.
Nimefurahi kusikia COSTECH wametufungulia mlango wa fursa ya kutukuza nami najiona mbali kwenye ulimwengu wa Teknolojia.
Leave a comment