Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia ‘aikopesha’ Dawasa Sh 500Mil. kusambaza maji Chalinze
Habari za Siasa

Samia ‘aikopesha’ Dawasa Sh 500Mil. kusambaza maji Chalinze

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema ametoa Sh. 500 Milioni kwaajili ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) kuanza kusambaza maji kwa wananchi wa Chalinze. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani … (endelea).

Rais Samia amebainisha hayo leo Jumanne tarehe 22 Machi 2022 wakati akizindua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze-Mboga, unaozalisha lita milioni 9.3 kwa siku.

Amesema maji hayo yanapaswa kuwafikia wananchi hivyo anatoa kiasi hicho cha fedha “kama mkopo” na kama usambazaji utafanyika vizuri ataongeza kiasi kingine kama hicho.

“Tunataka maji haya yawafikie wananchi kama mlivyosema wenyewe na kwa maana hiyo ndiyo nimetoa maelekezo tunaanza na Milioni 500 zinakuja Dawasa kuanza kazi ya uasmbazaji maji kwa wananchi,” amesema na kuongeza;

“Tunaanza na hizo na tunaangalia kasi yenu, kama kasi itakuwa nzuri tutaongeza nyingine 500 lakini hii fedha Dawasa mtakuja kuirudisha kwasababu wananchi wanawalipa nyie kwahiyo mtairudisha kwenye ule mfuko liotoa,”

Vilevile amewataka Dawasa kuweka mfumo mzuri wa usambazaji maji ili wananchi wote wafikiwe na maji.

“Nimefurahi kusikia kazi ya kusambaza maji kwa wananchi imeenza kwa kasi sas ingezeni kasi, ongezeni bidii kwani wananchi wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu kuipata huduma hii ya msingi,”

Aidha amewataka wananchi wa Chalinze kuilinda miundombinu ya mradi huo uliogharibu Sh 19 bilioni, ili iweze kuendelea kuwapatia maji kwani uharibifu wake utawakosesha maji.

Rais Samia pia amewasisitiza wananchi kulipa bili za maji ili mradi huo wenye uwezo wa kuhudumia wananchi 120, 972, uweze kuwa endelevu.

1 Comment

  • Kazi iendelee!
    Yule mchina aliyevuta maji na kuonyima Tanesco uwezo wa kutengeneza umeme vipi?
    Ahsante kwa kuwapa jukumu la kuitunza na kuilinda mitambo yao. Wasikubali wageni wawakaushie maji kama mambumbumbu.
    Wanaovuta maji lazima wapate kibali cha DAWASA na TANESCO ili wasiharibu uzalishaji wa umeme na usambazaji wa maji.
    Mama naomba uvunje mfumo wa kikoloni usiowashirikisha wananchi kwani wabunge wengi ni wasaliti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!