May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chama hashikiki VPL

Clatous Chama

Spread the love

 

KIUNGO wa Simba, Clatous Chama amekuwa na msimu bora mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuhusika katika mabao 20 kati ya mabao 58 waliyofunga Simba katika michezo 25 waliyocheza mpaka sasa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezaji huyo raia wa Zambia ambaye alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2019/20 huenda akajiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa tena tuzo hiyo kwa msimu huu.

Katika mchezo wa jana wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji, kiungo huyo alitoa pasi mbili za mabao (assist) katika ushindi wa mabao 3-1 walioupata Simba kwenye mchezo huo.

Kwa sasa mchezaji huyo anahusika kutoa pasi 13 zilizozaa mabao (assist) huku akiingia kambani mara saba na kuwa mchezaji ambayo amehusika katika mabao 20 yaliyofungwa na Simba katika msimu huu.

Chama kwa sasa anafukuzia rekodi ya Ibrahimu Ajibu aliyepiga pasi za mwisho 15 (assist) akiwa Yanga kwenye msimu wa 2018/19 na kumaliza msimu huo akiwa na mabao saba.

Simba kwa sasa imebakisha michezo tisa kukamlisha msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo mpaka sasa wapo kileleni wakiwa na pointi 61, mara baada ya kucheza michezo 25.

error: Content is protected !!