May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sare dhidi ya Chelsea, Zidane kuchukua maamuzi magumu

Zinedine Zidane

Spread the love

 

BAADA ya kutoka sare ya mabao 1-1, kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Chelsea, kocha wa Real Madrid huenda akawapumzisha wachezaji wake kwenye mchezo ujao wa La Liga dhidi ya Osasuna kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa mzunguko wa pili wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Chelsea utachezwa tarehe 5 Mei, 2021 kwenye Uwanja wa Stamford Bridge London, England.

Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari mara baada ya mchezo huo Zidane alisema kuwa kuelekea mchezo dhidi ya Osasuna siku ya Jumamosi wataangalia uwezekano wa kupunguza dakika watakazocheza wachezaji wake ili wawe katika hali nzuri kwa ajili ya mchezo wa marudiano.

“Tutaenda kuangalia, dakika tutakazoweza kuwapa kwa sababu tuna mchezo siku ya Jumamosi na tuwe katika hali nzuri kwa ajili ya marudiano,” alisema kocha huyo.

Aidha kocha huyo alizungumzia hali ya nahodha wa kikosi hicho, Sergio Ramos ambaye yupo majeruhi, amesema kuwa tayari amesharudi lakini bado hajafanya mazoezi na timu.

Ugumu wa kupumzisha wachezaji muhimu kwenye mchezo wa La Liga unakuja kufuatia timu hiyo kuwa katika mbio za ubingwa sambamba na klabu za Barcelona na Atletico Madrid.

Kwenye msimamo wa ligi hiyo, Real Madrid anashika nafasi ya pili akiwa na pointi 71, baada ya kucheza michezo 33, sawa na Barcelona iliyokuwa katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 71 na michezo 32, alama mbili nyuma ya kinara wa msimamo huo klabu ya Atletico Madrid mwenye pointi 73 akiwa na michezo 33.

Katika mchezo wa jana wa nusu fainali ambao Real Madrid walikuwa nyumbani, Chelsea walitangulia kupata bao kwenye dakika ya 14 ya mchezo kupitia kwa Christian Pulisic na dakika ya 28 Kareem Benzema alifanikiwa kusawazisha bao hilo.

error: Content is protected !!