Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yawaita CCM kwenye maandamano
Habari za Siasa

Chadema yawaita CCM kwenye maandamano

Maandamano Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewataka wanachama wa vyama vya siasa hususan Chama Cha Mapinduzi (CCM), kushiriki maandamano waliyoyaandaa kupinga ugumu wa maisha na kudai katiba mpya, kwa kuwa athari zake hazibagui mtu kulingana na itikadi zake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza…(endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 14 Februari 2024 na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Benson Kigaila, akizungumzia maandalizi ya awamu ya pili ya maandamano hayo ya amani yanayotarajiwa kufanyika kesho Alhamisi, jijini Mwanza.

“Chama chetu tumeamua kwa niaba ya Watanzania, ni kazi ya kufa na kupona kwa sababu ni lazima serikali ya watu isikilize watu. Hatuwezi kuwa na serikali ambazo hazisikilizi watu, Serikali kwenye demokrasia hafifu kama yetu zinawekwa na watu lazima zisikilize watu hivyo tunataka serikali hii iwasikilize watanzania,” amesema Kigaila.

Kigaila amesema “ugumu wa maisha hauchagui kabila wala itikadi za kisiasa wote tunacharazwa viboko vilevile sababuy masoko yetu yaleyale. CCM huwa wanajidanganya wakati wa kampeni wanasema wataisoma namba wanadhani tutaisoma sisi lakini tukimaliza uchaguzi na wenyewe wanashuka tunarudi nyuma tunaisoma namba CCm iko mbele kwa mbele.”

Kigaila amewataka viongozi wa vyama vya siasa kushiriki maandamano hayo ili kudai katiba mpya na kupinga miswada ya marekebisho ya sheria za uchaguzi ambayo imepitishwa bungeni hivi karibuni kwa ajili ya kuwa sheria baada ya kusainiwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

“Maandamano haya tumeamua tuandae kwa niaba ya watanzania wote wanaoteseka, yanalenga kila mtanzania mpenda haki na anayeumia. Tunawaalika taasisi zote bila kujali vyama vyao waje tuungane. Vyama vya siasa vyote waje tuungane sababu ni taasisi zilizosajiliwa kuusemea umma ukiwa kwenye shida,” amesema Kigaila.

Awamu ya kwanza ya maandamano hayo ilifanyika Januari mwaka huu jijini Dar es Salaam, ambapo msafara wake uliishia katika ofisi za Umoja wa Taifa (UN)nchini, zilizoko jijini humo, kisha kuwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya taasisi hiyo ya kimataifa kutoa wito kwa Serikali iyafanyie kazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!