Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Askofu Malasusa awataka viongozi wa kisiasa kumrudia Mungu
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Askofu Malasusa awataka viongozi wa kisiasa kumrudia Mungu

Spread the love

MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa, amewataka viongozi wa kisiasa kufanya ibada kulingana na imani zao ili waweze kuwaongoza vyema wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Askofu Malasusa ametoa wito huo leo Jumatano, akiongoza ibada fupi ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, katika Kanisa la KKKT Usharika wa Azania Front, ambapo amedai viongozi wa dini huwa na wakati mgumu kuwafanyia ibada ya mazishi viongozi wa kisiasa ambao enzi za uhai wao walikuwa hawashiriki ibada.

“Kiongozi wa watu ambaye anapenda ibada anamjua huyo Mungu aliyempa watu wa kuwaongoza, sasa mtu mwenye akili unaongoza watu walioumbwa na Mungu halafu huendi kwa Mungu kumsikia ili uongoze vizuri. Nawasihi kupitia ibada hii ya Lowassa hebu kwa kuwa Yesu hajarudi na tuanze kufikiri juu ya maisha ya ibada, haijalishi unasali wapi sikwambii uje wapi nenda kokote ambapo Mungu amekuongoza ili ukamwambie Mungu ahsante naomba unifanye kuwa kiongozi mzuri,” amesema Askofu Malasusa.

Kiongozi huyo wa kiroho amesema, KKKT halijapata wakati mgumu kumfanyia ibada Hayati Lowassa, aliyefariki dunia tarehe 10 Februari 2024, kwa kuwa alikuwa anashiriki enzi za uhai wake.

“Tusilazimishe miili kuileta tu hasa inapofikia hatua ya kulala kama hapa , leo tunapoongoza ibada hii hatuna dilemma katika kioyo yetu sababu tunajua tuko na mtu ambaye alipenda ibada na wakati mwingine mnapotulazimisha tunapata tabu, huyu anatakiwa kupigiwa makofi japo amelala,” amesema Askofu Malasusa.

Mbali na kumsifu Hayati Lowassa kwa kupenda Ibada, Askofu Malasusa amesema kifo chake ni msiba mkubwa ambao umegusa mioyo ya watu wengi.

Naye msemaji wa famila ya Lowassa, ambaye ni mtoto wa mwanasiasa huyo, Fred Lowassa, amesema enzi za uhai wake aliwafundisha nidhamu ya kuheshimu na kushiriki siku za ibada.

“Kama ambayo wengi sehemu ambayo baba muda wote alipokuwa na nguvu alikuwa anakuja siku ya Jumapili hakosi na ametufundisha nidhamu hiyo hata siku ambayo sisi tunaamka hatuendi kanisani unamuona kama anakuangalia wewe vipi unafanya nini leo?” amesema Fred.

Mwili wa Lowassa aliyezaliwa 1953, unatarajiwa kuzikwa nyumbani kwao Monduli, jijini Arusha, tarehe 17 Februari mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

error: Content is protected !!