Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano
Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Maandamano Chadema
Spread the love

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya pili ya maandamano ya amani yanayotarajiwa kufanyika tarehe 22 hadi 30 Aprili 2024, yatafanyika kwenye kanda nne. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Alhamisi, jijini Dar es Salaam, Mkrugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje Chadema, John Mrema, amezitaja kanda hizo kuwa ni za Kaskazini, Victoria, Serengeti na Kati.

Mrema amesema maandamano hayo yatakuwa na misafara miwili, itakayoongozwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara, Tundu Lissu.

Amesema msafara wa Mbowe utaanza tarehe 22 Aprili 2024, Kanda ya Victoria mkoani Kagera, kisha siku inayofuata msafara huo utaongoza maandamano ya mkoani Shinyanga.

Tarehe 24 Aprili 2024, Mbowe na msafara wake utaongoza maandamano ya Geita Mjini. Msafara huo utahimisha maandamano hayo tarehe 30 Aprili mwaka huu, mkoani Kilimanjaro.

Msafara wa Lissu utaanzia Kanda ya Kaskazini jijini Arusha, Kisha kuhitimishwa Kanda ya Kati mkoani Morogoro.

Mrema amesema ajenda zitakazoteka maandamano hayo ni ugumu wa maisha, kikokotoo Cha mafao ya wastaafu, madai ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Katika awamu ya pili Chadema kimepanga kufanya maandamano katika Kanda zote, wakati awamu ya kwanza yalifanyika katika majiji ya Mbeya, Mwanza, Arusha na Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!