Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe
Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi
Spread the love

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti wa umoja wake wa vijana (UVCCM), mkoani Kagera, Faris Buruhan, ya kuwapoteza wapinzani wanaotuka viongozi mtandaoni. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na wanachama wa CCM mkoani Mbeya, Jana tarehe 17 Aprili 2024, Karibu Mkuu wa CHAMA hicho, Dk. Emanuel Nchimbi amesema wanapinga kauli hiyo kwa kuwa ni ya kijinga.

Dk. Nchimbi alisema Kila mtu ana haki katika nchi ya Tanzania kwa kuwa sio ya vyama vya siasa, kidini au kikabila.

“Na Leo akiinuka kijana wa CCM kwa mfano akasema wapinzani wetu wakifanya hili na hili lazima tuwapoteze, huyu ni kijana wetu kaongea jambo la kijinga kwa sababu mwisho wa siku nchi ni yetu sote,” alisema Dk. Nchimbi

Tarehe 16 Aprili 2024, Buruhan alinukuliwa na vyombo vya habari akisema wakiwapoteza watu wanaotukana viongozi mitandaoni, polisi wasihangaike kuwatafuta.

Dk. Nchimbi alisema Kuna wakati viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wanasema jambo la maana.

“Ndio maana viongozi wa upinzani wakiwa katika mkutano wa hadhara Mwanza walimsifu Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kazi aliyofanya kuleta mshikamano na utulivu katika nchi yetu na katika Hilo hatuwezi kusema halina maana hata kama alisema wa upinzani,” alisema Dk. Nchimbi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!