Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yamtwisha zigo la ushindi Kikwete mikoa ya Kusini
Habari za Siasa

CCM yamtwisha zigo la ushindi Kikwete mikoa ya Kusini

Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Spread the love

CHAMA tawala nchini Tanzania cha Mapinduzi (CCM) kimesema, kimempeleka Rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete katika mikoa ya Kusini, ili akamalize wavurugaji wa chama hicho hususan mkoani Lindi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Lindi … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa tarehe a Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM wakati akizungumza na waandishi wa habari wilayani Chato Mkoa wa Geita kuhusu mikakati ya ushindi ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

Polepole amesema, CCM kimemchagua Kikwete aliyekuwa Rais wa Tanzania kati ya mwaka 2005-2015 kufanya kampeni mikoa ya Kusini, kwa kuwa anazifahamu vyema siasa za ukanda huo.

“Kikwete yeye yuko na Ukanda wa Kusini, anashambulia kwa hali ya juu, unajua kampeni ni sayansi na mikakati pahala ambako unaona watu wavurugaji unaweka watu wanaowafahamu vizuri, Kikwete tumemuweka Lindi ili kama kuna watu wanavuruga anawashughulikia zaidi,” amesema Polepole.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, CCM ilichuana vikali na upinzani ambapo waligawana majimbo karibu uwiano sawa na wabunge.

Jakaya Kikwete, Rais mstaafu wa Tanzania

Kuhusu mikakati ya ushindi ya chama hicho, Polepole amesema, katika uchaguzi huu CCM imeboresha kampeni zake kwa kugawanya makada wake waandamizi katika maeneo tofauti tofauti kwa ajili ya kushambulia kila kona.

“Kampeni zinafanywa kitofauti kidogo, mwaka huu  kampeni za CCM zinafanyika kisayansi ikizingatia weledi wa hali juu sana, chama kimegawanya makada waandamizi na viongozi katika maeneo mbalimbali ya nchi tuanshambulia kila kona,” amesema Polepole.

Akitangaza safu hiyo ya ushindi, Polepole amesema safu ya kwanza ni ya Mgombea Urais wa Tanzania, John Magufuli, ya pili ikiwa ni ya Mama Samia Suluhu Hassan, mgombea mwenza wakati ya tatu ikiwa ni ya Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu.

Safu ya nne inaongozwa na Kikwete huku safu ya tano ikiongozwa na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda, akishirikiana na Spika wa Tanzania Job Ndugai.

“Tutaimaliza nchi hii awamu hii yote halafu tutapiga raundi nyingine kipindi hicho nadhani pumzi ya wenzetu itakuwa imekata, sababu miaka mitano tumejenga taasisi imara sana ya CCM yenye uwezo kwa maana ya makada madhubuti, wanachama wameimarika na idadi yao imeongezeka maradufu,” amesema Polepole.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

Habari za SiasaTangulizi

‘Aliyemtonya’ Lissu kuhusu rushwa arejea madarakani

Spread the loveMwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Tutaendelea kupigania malengo ya afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NHC yadai bil. 2.1 taasisi za Serikali, Waziri atoa maagizo

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii...

error: Content is protected !!