LICHA ya kinyang’anyiro cha wagombea Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020 kuwa na wagombea 15, Tundu Lissu miongoni mwa wagombea hao kupitia Chadema amesema, wanaotikisa ni yeye na John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Bagamoyo … (endelea).
Lissu ambaye ni Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ametoa kauli hiyo jana Alhamisi tarehe10 Septemba 2020 wakati akizungumza katika kampeni zake wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Makamu huyo Mwenyekiti wa Chadema Bara alisema, katika uchaguzi huo, itakuwa ni ama zake au za Magufuli ambaye ni Rais wa Tanzania.
“Wagombea tuko 15 nasikia, lakini ukweli ni kwamba, hii biashara hii ya urais wa mwaka huu ni ya Magufuli na Tundu Lissu, ama zake ama zangu, ama za Magufuli ama za Tundu Lissu,” alisema Lissu huku akishangiliwa na umati wa wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo.

Wagombea wengine ni; Queen Cuthbert Sendiga (ADC), Bernard Membe (ACT-Wazalendo), Prof. Ibrahim Lipumba (CUF), Cecilia Mwanga (Demokrasia Makini), Hashimu Rungwe (Chaumma) na Seif Maalim Seif (AAFP).
Pia wamo, John Shibuda (Ada-Tadea), Yeremia Kulwa Maganja (NCCR-Mageuzi), Philipo Fumbo (DP), Leopard Mahona (NRA), Mutamwega Magaywa (SAU), Twalib Kadege (UPDP) na Maisha Mapya Muchunguzi wa NLD.
Kampeni za uchaguzi huo zinaendelea kwa vyama kunadi ilani kwa Watanzania na zitahitimishwa tarehe 27 Oktoba 2020.
Hapana Bwana wagombea wote 15 bado wana nafasi. Kitajulikana Siku tukipiga kura na zikahesabiwa vizuri na kwa usahihi bila mizegwe.
Nawatakia wote kampeni njema.
Kussagaibrahim@gmail.com
Tunaombea uchaguz uwe na Aman na huru na hali.
U selfish hautakiwe ni unafiki Mungu hampendi kabisa
Kuna maisha baada ya uchaguzi
Mjinga tu huyo tundu lissu hana sera za maana
Niambie